WAFUGAJI NCHINI WATAKIWA KUFUGA KISASA

Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki akizungumza wakati
wakati wa hafla ya kukabidhi malori na vifaa vya maziwa kutoka shirika la Heifer International kupitia mradi wa usindikaji maziwa Tanzania (TMPP) iliyofanyika katika kiwanda cha Tanga Fresh kilichopo Jijini Tanga kushoto aliyekaa ni Meneja wa Kanda ya Mashariki Benki ya Maendeleo ya kilimo TADB Jeremiah Mhada

Mkurugenzi wa mradi wa usindikaji wa maziwa Tanzania kutoka shirika la Helfer Mark Tsoxoakizungumza wakati wa halfa hiyo
Meneja wa Kanda ya Mashariki Benki ya Maendeleo ya kilimo TADB Jeremiah Mhada akieleza jambo wakati wa halfa hiyo
Kaimu Msajili bodi ya maziwa Noely Byamunguakizungumza wakati wa halfa hiyo
Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki kushoto akikata utepe wakati wa hafla ya kukabidhi malori na vifaa vya maziwa kutoka shirika la Heifer International kupitia mradi wa usindikaji maziwa Tanzania (TMPP) iliyofanyika katika kiwanda cha Tanga Fresh kilichopo Jijini Tanga kulia ni Mkurugenzi wa mradi wa usindikaji wa maziwa Tanzania kutoka shirika la Helfer Mark Tsoxo

Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki kushoto akimshukuru Mkurugenzi wa mradi wa usindikaji wa maziwa Tanzania kutoka shirika la Helfer Mark Tsoxo mara baada ya makabidhiano hayo kulia anayeshuhudia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ambaye pia alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga katika halfa hiyo
Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki akiwasha moja ya magari hayo

WAFUGAJI  nchini wametakiwa kubadilika na kuachana na ufugaji wa mazoea bali wafuge kisasa kwa ajili ya kupata mazao mengi lakini yenye ubora ambayo yataweza kuuzika kwa faida na hivyo kuongeza mchango wa pato la Taifa.

Ushauri huo umetolewa na Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki wakati wa hafla ya kukabidhi malori na vifaa vya maziwa kutoka shirika la Heifer International kupitia mradi wa usindikaji maziwa Tanzania (TMPP) iliyofanyika katika kiwanda cha Tanga Fresh kilichopo Jijini Tanga.

Alisema kuwa licha ya Tanzania kuwa na mifugo mingi lakini sekta hiyo mchango wake kwenye pato la taifa ni asilimia 7.9% pekee  kutokana na ufugaji wa kimazoea  ambao hautoi matokeo bora.

Akizungumzia uzalishaji wa maziwa nchini Waziri Ndaki alisema ni lita Bil 3.01 huku kati ya hizo lita Mil 2.1 zinatokana na ng'ombe wa asili Mil 31 huku ng'ombe wa kisasa Mil 2 wanatoa lita bil 0.9. 

"Kutokana na uzalishaji mdogo wa maziwa hata kiwango cha unywaji wa maziwa kwa mwananchi mmoja mmoja kimekuwa kidogo kwani kwa mujibu wa takwimu ni lita 54 kwa mwaka sawa na kijiko kimoja kwa siku" alisema Waziri Ndaki.

Nae Kaimu Msajili bodi ya maziwa Noely Byamungu alisema kuwa uwepo wa mradi umesaidia kuongeza kasi ys uanzishwaji wa viwanda vya maziwa hadi kufikia vitano ambavyo vinazalisha maziwa kwa kutumia teknolojia ya UHT.

Alisema kuwa bado kumekuwepo na changamoto katika eneo la ukusanyaji wa maziwa kwani kuna kiasi kikubwa yanakuwa hana kosa ubora kabla ya kufika soko hivyo kuwa hasara kwa mfugaji.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uzalishaji na masoko kutoka wizara ya mifugo na uvuvi Steven  Maiko alisema kuwa kutokana na tathimini waliyoifanya 2016/17 inaonyesha kuwa ifikapo mwala 2030/31 sekts hiyo itakabiliwa na upungufu mkubwa raslimali zake za nyama na maziwa kutokana na ongezeko la idadi ya watu.

Hivyo kutokana na changamoto hiyo serikali kwa kushirikiana na wahisani waliamua kuja na mradi huo ili  kuongezs uzalishaji, kudhibiti magonjwa ya mifugo lakini.na kuongeza mnyororo wa thamani wa maziwa ikiwemo kuweka mazingira safi ya kufanyabiashara.

Nae  Mkurugenzi wa mradi wa usindikaji wa maziwa Tanzania kutoka shirika la Helfer Mark Tsoxo alisema kuwa lengo la mradi wa TMPP kuongeza kipato kwa wafugaji wapatao 50, 000 nchi nzima na kwa kipindi cha miezi mitatu pekee tayari wameweza kuwafikia wafugaji 45, 000 kwa kuwapa mafunzo ya ufugaji wa kisasa ili waweze kupata mazao bora na ambayo yataweza kuuza kwa urahisi.

Alisema kwa upande wa wasindikaji waweze kuwawezesha vifaa ili kuhakikisha wanaboresha ukusanyaji wa maziwa na kudhibiti ubotevu wake ili kumuhakikishia mfugaji  soko lenye uhakika.

Nae Meneja wa Kanda ya Mashariki Benki ya Maendeleo ya kilimo TADB Jeremiah Mhada alisema kuwa benki hiyo imewawezesha wafugaji mkopo wa zaidi ya sh Mil 396 pamoja na mitamba bora.

"Ili kuongeza kipato kwa wafugaji wadogo tumewawezesha kupata mitamba ya kisasa na kiwaunganisha ns masoko ili kuongeza thamani na kuchoches kuongeza uzalishaji wa maziwa nchini" alisema Mhada.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments