MVUA YALETA MADHARA SONGEA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, January 19, 2021

MVUA YALETA MADHARA SONGEA

  Malunde       Tuesday, January 19, 2021


Mvua mkubwa iliyoambatana na upepo imesababisha maafa ya kuezuliwa paa katika madarasa matano, ofisi mbili na stoo moja kwenye shule ya msingi ya Mfaranyaki iliyopo manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma, – Simon Maigwa amesema tukio hilo limetokea jana majira ya saa tisa mchana, ambapo mvua hiyo ilidumu kwa takribani dakika 30.

Kamanda Maigwa amesema licha ya kuezua paa katika madarasa hayo matano, mvua hiyo pia imesababisha madhara kwa kaya tisa ambapo saba ni katika mtaa wa CCM kata ya Mjini na nyumba nyingine mbili za familia za polisi katika kituo kikuu nazo zimeezuliwa paa.

Amesema mvua hiyo pia imeezua paa katika baadhi ya vibanda vya biashara kwenye soko kuu la Songea huku tathmini ya madhara hayo ikiendelea kufanyika.

Diwani wa kata ya Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)katika Manispaa ya Songea Mathew Ngalimanayo amesema hakuna kifo chochote kilichoripotiwa kufuatia mvua hizo.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post