MAREKANI YAITUHUMU IRAN KUWA NI 'KAMBI MPYA' YA MTANDAO WA AL-QAEDA | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, January 13, 2021

MAREKANI YAITUHUMU IRAN KUWA NI 'KAMBI MPYA' YA MTANDAO WA AL-QAEDA

  Malunde       Wednesday, January 13, 2021


Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Mike Pompeo ameituhumu Iran kwa kuwa na ushirikiano wa ksiri ya mtandao wa al-Qaeda. 

Kutokana na madai hayo, Pompeo amewawekea maafisa kadhaa wa Iran vikwazo.

Kwenye hotuba yake kwa waandishi wa Habari, Pompeo aliishutumu Iran kwa kuwa na uhusiano wa siri na al-Qaeda huku akitaja duru za ujasusi zinazodai kuwa Iran ilimhifadhi kiongozi wa pili wa mtandao huo Abu Muhammad al-Masri ambaye aliuawa mwezi Agosti na mawakala wa Israel.

 Kauli ya Pompeo imejiri wiki moja tu kabla ya utawala wa Trump kuondoka ofisini, na inaonekana kulenga nia ya rais mteule Joe Biden kuanzisha mazungumzo na Iran kuhusu makubaliano ya mwaka 2015 ya mpango wa nyuklia. 

Rais Donald Trump aliiondoa Marekani kwenye mkataba huo mwaka 2018.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post