BASATA YAMFUNGIA GIGY MONEY KUTOJIHUSISHA NA MASUALA YA BURUDANI NA SANAA


Msanii Gigy Money

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemfungia msanii Gigy Money kwa kutojihusisha na masuala ya burudani na sanaa kwa muda wa miezi 6 pamoja na faini ya Milioni 1 kwa kosa la kudhalilisha utu wake kuonesha maungo yake ya mwili.

BASATA wametoa taarifa hiyo kufuatia tukio la msanii huyo kupanda jukwaani kwa ajili ya kutumbuiza kisha akavua gauni lake na kubakia na dela, vazi ambalo lilikuwa linaonesha maungo yake ya ndani ya mwili hivyo alibugudhi hadhira ya wapenda sanaa ndani na nje ya Tanzania.

Aidha BASATA wamesema walishamuita msanii huyo kwa ajili ya kumuonya vitendo hivyo vya ukiukwaji wa sheria za maadili na aliahidi kutorudia tena, pia Baraza linawakumbusha wasanii wote hapa nchini kufanya sanaa kwa kuzingatia sheria, kanuni, na taratibu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post