MITANDAO YA KIJAMII YAZIMWA MKESHA WA UCHAGUZI UGANDA

Mamlaka nchini Uganda ilikatiza hudama za intaneti saa kadhaa kabla ya uchaguzi wa urais unaokumbwa na ushindani mkali kati ya nyota wa muziki na mmoja viongozi wa muda mrefu wa Afrika waliohudumu miaka mingi madarakani.

Kundi la ufuatiliaji wa masuala ya Intaneti NetBlocks liliandika kwenye Twitter yake kwamba nchi hiyo ilizima mitandao yote ya intaneti Jumatano saa moja usiku majira ya Afrika Mashariki.

Hatua hiyo ilifuatia agizo la serikali kufungia mitandao yote ya kijamii na programu tumishi za kutuma ujumbe.

Rais Yoweri Museveni alisema alifikia uamuzi huo kwa sababu Facebook ilifunga akaunti kadhaa zinazounga mkono chama tawala.

Mgombea wa urais,mwanamuziki aliyegeuka Bobi Wine aliandika katika Twitter yake kwamba huduma za intaneti zimekatizwa kama sehemu ya njama ya kuiba kura.

"Watu wa Uganda wako imara na hakuna jambo lolote litakatiza azma yao ya kikomesha utawala wa kiimla," aliongeza.

Shughuli za upigaji kura ilianza saa moja asubuhi ya leo Alhamisi, japo matokeo hayatarajiwi kutolewa kabla ya Jumamosi.

Kampeni za uchaguzi zilikumbwa na ghasia ambazo zilisababisha vifo vya makumi ya watu.

Bw. Museveni anagombea muhula wa sita baada ya kuwa madarakani kwa miaka 35.

 CHANZO - BBC SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments