KAIMU MKURUGENZI ASIMAMISHWA KAZI KWA KUSAFIRISHA MAITI YA MTUMISHI JUU YA GARI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amemuagiza Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Mhandisi Joseph Nyamuhanga kumsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara Jumanne Yassin ili kupisha uchunguzi, kufuatia kitendo cha halmashauri hiyo kusafirisha mwili wa Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Emmanuel Sizo juu ya Carrier ya gari.

Waziri Jafo ametoa agizo hilo baada ya gari iliyobeba mwili wa Mtumishi huyo.kusambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Amesema amesikitishwa na kitendo hicho ambacho ni kinyume na kanuni za utumishi wa Umma, pamoja na mila na desturi za Mtanzania.

Ameagiza Watumishi wote waliohusika na uzembe huo wachukuliwe hatua za kinidhamu kwa mujibu wa sheria, kanuni.na taratibu za utumishi wa Umma.

Waziri Jafo amewataka Watumishi wote wa Umma katika tawala za mikoa na mamlaka za serikali za mitaa kujenga tabia ya kuheshimiana, kupendana na kuthaminiana wakati wote wanapotekeleza majukumu yao.

Sizo alifariki duniani kwa ajali ya gari mkoani Singida Januari 10 mwaka huu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post