Tanzia : ALIYEKUWA RC KIGOMA BRIGEDIA JENERALI MSTAAFU EMMANUEL MAGANGA AFARIKI DUNIA


 Brigedia Jenerali mstaafu, Emmanuel Maganga enzi za uhai wake.
***
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali mstaafu, Emmanuel Maganga amefariki dunia leo Alhamis usiku Januari 21,2021.

Taarifa za awali zinasema kuwa Brigedia Jenerali mstaafu, Emmanuel Maganga amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Jeshi mkoani Tabora.

Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga alistaafu mwezi Julai, mwaka 2020 ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alimteua Bw. Thobias Andengenye (aliyewahi kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji) kuwa Mkuu wa mkoa wa Kigoma kuchukua nafasi ya Brig. Gen. (Rtd) Emmanuel Maganga.

 BWANA AMETOA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments