AFARIKI KWA KUKANYAGWA NA TRENI AKIDANDIA


Picha ya mfano wa treni

Na Mwandishi wetu  - Moshi
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Noa amefariki dunia baada ya kukanyagwa na treni ya abiria akiidandia wakati ikiwa imeanza kuondoka katika stesheni ya Moshi mkoani Kilimanjaro. 

Noa anayedaiwa kuwa fundi ujenzi aliyekuwa akitoka Dar es Salaam kwenda Arusha amekanyagwa na treni wakati akijaribu kudandia treni hiyo iliyokuwa ikitoka Dar es Salaam kwenda Arusha leo Alhamis Januari 21,2021.

Kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro Ronald Makona amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa treni hiyo ilipofika Stesheni ya Moshi, Noa alishuka na kwenda kujisaidia na hivyo treni hiyo kumuacha na alipojaribu kuikimbiza ili apande kwenye behewa lake kwa bahati mbaya aliteleza na ikamkanyaga na kumkata vipande.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post