ASKARI POLISI AWANUNULIA CHAKULA WATUHUMIWA WA WIZI BADALA YA KUWAKAMATA


Afisa mmoja wa polisi ambaye alikuwa ameitwa kuikamata familia moja inayoshukiwa kuiba katika duka moja badala yake aliwanunulia chakula ili waweze kusherehekea chakula cha jioni cha Krismasi.

Matt Lima aliitwa katika duka moja la chakula katika eneo la Somerset , Massachussetts , mwezi uliopita , taarifa ya polisi ilisema.

Wanawake wawili walidaiwa kutoweka katika mashine ya skani vitu vyote walivyonunua katika duka hilo.

Walipoulizwa, familia hiyo ilisema kwamba haikuweza kulipia kila kitu walichokuwa wakihitaji kutokana na hali mbaya ya kiuchumi.

Hata hivyo walisema kwamba walikuwa wanafanya hivyo ili kuwatengenezea chakula kizuri cha krismasi watoto wao.

Bwana Lima aliwakamata lakini hakuwafungulia mashtaka kwa kuwa kila walichokuwa wamenunua kilikuwa chakula , polisi walisema.

Baadaye aliwanunulia kadi za zawadi zenye thamani ya $250 na fedha zake binafsi ili wanawake hao na watoto wao wawili kuweza kununua chakula cha krisimasi katika duka jingine la kampuni kama hiyo.

''Watoto hao wawili na wanawake hao walinikumbusha watoto wangu , hivyo basi nililazimika kuwasaidia'' , alisema afisa Lima.

''Ukweli ni kwamba familia hii ilikuwa inahitaji chakula hivyo basi siwezi kufikiria kufanya uamuzi kwenda katika duka la Stop and Shop na kununua kile ninachoweza kununua pekee - ama niende na kujaribu kununua chakula cha krismasi cha watoto hao''? aliambia runinga ya eneo hilo.

''Walinishukuru sana , mwanzo walikuwa wameshangaa. Nina hakika watu wengi walio katika hali hiyo wangefikiria kwamba kungekuwa na tukio tofauti na pengine wangekamatwa na kupelekwa mahakamani''.

''Nilinunua kadi ya thamani ya kile ambacho kingechukuliwa'', aliongezea.

''Nilifanya kile nilichoona ni sawa. Sio jambo la kunihusu nilijiweka katika viatu vya familia na kuonyesha huruma kidogo''.

CHANZO - BBC SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post