NANCY PELOSI ACHAGULIWA TENA KUWA SPIKA WA BARAZA LA WAWAKILISHI MAREKANI | MALUNDE 1 BLOG

Monday, January 4, 2021

NANCY PELOSI ACHAGULIWA TENA KUWA SPIKA WA BARAZA LA WAWAKILISHI MAREKANI

  Malunde       Monday, January 4, 2021


Bunge la Marekani limewachagua viongozi wake wapya, wiki mbili na nusu tu kabla ya rais mteule Joe Biden kuchukua madaraka rasmi.
 

Kwa mara nyingine Baraza la Wawakilishi limemchagua Nancy Pelosi kuwa Spika wake, japo kwa kura chache ikilinganishwa na muhula uliopita. 

Kwa uchaguzi huo Bi Pelosi mwenye umri wa miaka 80 anaendelea kushikilia mojawapo ya ofisi zenye mamlaka makubwa kabisa nchini Marekani.

 Hata wajumbe wa Baraza la Seneti walikula kiapo, lakini uongozi wa baraza hilo utajulikana bayana baada ya uchaguzi wa marudio wa majimbo mawili ya ubunge katika jimbo la Georgia ambao unafanyika kesho Jumanne. 

Matokeo ya uchaguzi huo ndio yataamua uwezo atakaokuwa nao rais mpya katika kupitisha sera zake.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post