Tanzia : MBUNGE WA CCM AFARIKI DUNIA


Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Manyara, Martha Umbulla amefariki dunia katika Hospitali ya HCG Mumbai, India alikokuwa akipatiwa matibabu.
Kifo cha mbunge huyo aliyezaliwa Novemba 10, 1955 kimetangazwa leo Alhamisi Januari 21, 2021 na Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ambaye amesema mbunge huyo amefariki dunia jana Jumatano Januari 20, 2021 

“Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Martha Umbulla. Natoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, wabunge na wananchi wa Mkoa wa Manyara. Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu.
“Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi amina,” amesema Ndugai.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi mjini Babati Feisal Dauda pia amethibitisha kutokea kwa kifo cha Mbunge wa viti maalum mkoa wa Manyara Martha Umbura amefariki dunia.

Taarifa hiyo ambayo katibu wa CCM Mjini Babati ameipakia katika ukurasa wake binafsi wa Facebook, haijaeleza chanzo cha kifo chake.

Martha Umbura amekuwa Mbunge wa viti maalum mkoa wa Manyara zaidi ya miaka kumi ambapo hadi anafariki alikuwa Mbunge wa viti maalum katika mkoa huo.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, Amina.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post