AKAMATWA BAADA YA KUNASWA AMEFICHA MWILI WA MAREHEMU MIAKA 10 NYUMBANI


Polisi nchini Japan wamemkamata mwanamke mmoja baada ya mwili wa mama yake kukutwa kwenye jokofu nyumbani kwake.

Yumi Yoshino, 48, amesema kuwa alimkuta mama yake akiwa amefariki dunia kisha aliuficha mwili wake miaka 10 iliyopita kwa sababu '' hakutaka kuhama'' katika nyumba waliokuwa wakiishi mjini Tokyo, vyombo vya habari vimewanukuu maafisa polisi ambao hawakutajwa majina yao.

Hakukuonekana majeraha yoyote kwenye mwili ulioganda barafu, polisi wameeleza.

Mamlaka hawakuweza kuthibitisha muda na sababu ya kifo cha mwanamke huyo.

Mwili uliripotiwa kugundulika na mfanya usafi baada ya Bi. Yoshino kulazimishwa kuondoka katika nyumba hiyo kwa sababu ya kukosa kodi.

Mwili ulikuwa umekunjwa kiasi cha kutosha kuingia kwenye jokofu lenye barafu, polisi walisema.

Bi Yoshino alikamatwa katika hoteli mjini Chiba karibu na jiji la Tokyo, siku ya Ijumaa.

CHANZO - BBC SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments