RAIS MAGUFULI AONGOZA VIONGOZI NA WANANCHI KUAGA MWILI WA JAJI MSTAAFU HAROLD NSEKELA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, December 8, 2020

RAIS MAGUFULI AONGOZA VIONGOZI NA WANANCHI KUAGA MWILI WA JAJI MSTAAFU HAROLD NSEKELA

  Malunde       Tuesday, December 8, 2020


Rais Dkt. John Magufuli ameongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela aliyefariki dunia Disemba 6 mwaka huu jijini Dodoma.

Shughuli ya kuaga mwili wa Jaji Mstaafu Nsekela imefanyika katika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Viongozi mbalimbali wameshiriki katika shughuli hiyo akiwemo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma.

Mara baada ya kukamilika kwa shughuli hiyo ya kuaga mwili wa Jaji Mstaafu Nsekela mwili huo umesafirishwa kwa ndege kwenda mkoani Mbeya kwa mazishi, yatakayofanyika Alhamisi Disemba Kumi.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post