KAULI YA MAALIM SEIF SHARIF HAMAD BAADA YA KUAPISHWA LEO KUWA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, December 8, 2020

KAULI YA MAALIM SEIF SHARIF HAMAD BAADA YA KUAPISHWA LEO KUWA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR

  Malunde       Tuesday, December 8, 2020

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad ameahidi kuwatumikia Wananchi wa Zanzibar akiwa katika wadhifa huo.

Akizungumza mara baada ya kuapishwa kushika rasmi wadhifa huo Ikulu jijini Zanzibar, Maalim Seif amewashukuru Wananchi wa Zanzibar kwa imani kubwa walioionesha kwake.

Maalim Seif ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha ACT Wazalendo, amekishukuru chama chake kwa kumpendekeza kuwa Makamu wa Rais wa Zanzibar.

Amesema uamuzi wa Chama Cha ACT Wazalendo kuingia katika serikali ya Umoja wa Kitaifa haukuwa rahisi, lakini waliamua kuuridhia kutokana na dhamira ya dhati ya Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi ya kushirikian na chama hicho.

Amewataka Wananchi wote wa Zanzibar wa ndani na nje, kushirikiana ili kuijenga Zanzibar na ameahidi kushirikiana na Rais Mwinyi.

Disemba 6 mwaka huu Rais Mwinyi alimteua Maalim Seif Sharif Hamad kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post