JOE BIDEN: TRUMP AMEHARIBU IDARA MUHIMU ZA USALAMA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, December 29, 2020

JOE BIDEN: TRUMP AMEHARIBU IDARA MUHIMU ZA USALAMA

  Malunde       Tuesday, December 29, 2020


Vitengo muhimu vya usalama vimefanyiwa uharibifu mkubwa chini ya utawala wa rais Donald Trump , rais mteule wa Marekani Joe Biden amesema.
 

Biden amesema kwamba timu yake haipati habari inazohitaji kutoka kwa idara ya ulinzi wakati ambapo inajiandaa kuchukua madaraka.
 

Kiongozi huyo mteule ametoa kauli hiyo wakati akizungumza baada ya kupatiwa habari na Maafisa wa Usalama pamoja na wale wa masuala ya sera za kigeni.

Biden anatarajiwa kuapishwa Januari 20, mwakani kuwa rais, hata hivyo Rais Trump amekataa kukubali kushindwa katika uchaguzi wa mwezi Novemba.

Kwa wiki kadhaa baada ya uchaguzi huo wa Novemba 3 , Biden alizuiliwa kupata habari muhimu za kijasusi , ikiwa ni muhimu na utaratibu wa kawaida katika mchakato wa kumkabidhi rais mteule madaraka.

Kufuatia matamshi ya Joe Biden siku ya Jumatatu , kaimu waziri wa ulinzi Christopher Miller amesema kwamba maafisa wamekuwa wakifanya kazi kwa utaalamu mkubwa kuunga mkono mpito.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post