AINA MPYA YA KIRUSI CHA CORONA YARIPOTIWA MAREKANI | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, December 30, 2020

AINA MPYA YA KIRUSI CHA CORONA YARIPOTIWA MAREKANI

  Malunde       Wednesday, December 30, 2020

 


Aina mpya ya kirusi cha corona kinachoaminka kusambaa kwa kasi, imeripotiwa kwa mara ya kwanza nchini Marekani na Amerika ya Kusini


Aina hiyo mpya ya kirusi cha corona kilichogunduliwa kwa mara ya kwanza nchini Uingereza, sasa kimeripotiwa kuingia Marekani katika mji wa Colorado. 

Kirusi hicho kimegundulika kwa kijana wa miaka 20 ambaye hana historia ya kusafiri. 

Taarifa za vyombo vya habari za ndani zinasema kuna uwezekano wa kisa kingine cha kirusi hicho. 

Wataalamu wanaamini kwamba aina hiyo mpya inaweza kuenea kwa kasi na itakuwa chanzo cha ongezeko la maambukizi Uingereza. 

Aina hiyo mpya ya kirusi kinachujulikana kama B.1.1.7 tayari pia imeripotiwa Canada, Italia, India na Umoja wa Falme za Kiarabu. Chile nayo imeripoti aina hiyo mpya na kulifanya kuwa taifa la kwanza Amerika ya Kusini kubaini maambukizi yake.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post