MAHAFALI YA 50 UDSM YAFANYIKA....WAHITIMU WASHAURIWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUJIAJIRI


Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwatunuku shahada mbalimbali wahitimu wa Chuo hicho Jijini Dar es Salaam. Wahitimu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam wakiwa katika Ukumbi wa Mahafali ya 50 yaliyofanyika Mlimani City Jijini Dar es Salaam. 

********************

NA EMMANUEL MBATILO 

Wahitimu katika wa elimu ya juu wametakiwa kutokusubiri kuajiriwa na Serikali na badala yake kuangalia ni wapi ujuzi wao unaweza kutumika kwa ufanisi zaidi. 

Hayo yameelezwa katika sherehe za mahafali ya 50 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ( UDSM ) Kampasi ya Mwalimu Julius Nyerere wakati wa utoaji wa Shahada za wahitimu waliofuzu na kustahili kutunikiwa. 

Akizungumza katika Mahafali hayo Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Prof.William Anangisye amewataka wahitimu hao kuwa watu wa kutafuta fursa badala ya fursa ziwafuate jambo ambalo si rahisi kutokea katika ulimwengu wa leo. 

"Mtakapokuwa mnatekeleza wajibu wenu wa kujitafutia maisha mazuri na kuendeleza nchi yetu, muwe na hulka ya kuthubutu kujaribu mambo ambayo yanaonekana ni magumu" Amesema Prof.Anangisye. 

Aidha amesema Serikali imeendelea kugharamia na kudhamini mafunzo ya wafanyakazi wa kada mbalimbali na kuwapa stahiki zao muhimu za kiutumishi. 

"Serikali imeendelea kujenga na kuboresha miundombinu muhimu na kutoa fedha kwa ajili ya kugharamia uendeshaji wa Chuo kwa ujumla". Amesema Prof.Anangisye. 

Nao baadhi ya wahitimu katika Shahada za awali wakizungumza na kituo hiki katika mahafali hayo wamesema wanapongeza juhudi za chuo kikuu cha Dar es Salaam na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutatua changamoto mbali mbali zilizopo chuoni, ikiwemo ujenzi wa maktaba mpya,ujenzi wa mabweni ya J.P Magufuli na uimarishaji wa miondombinu ya kufundishia huku wakibainisha changamoto ya uhaba wa mabweni,upungufu wa vifaa vya kujifunzia kwa vitendo kwenye kozi za sayansi,uhandisi na teknolojia. Mahafali hayo ya 50 ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Kampasi ya Mwalimu Julius Nyerere Jumla ya wahitimu 10,668 kutoka katika Shahada mbalimbali wametunukiwa Shahada zao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post