MANISPAA YA SHINYANGA, WADAU WAADHIMISHA KILELE CHA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA


 

Afisa Maendeleo ya jamii halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone (katikati), akikabidhi taulo za kike kwa viongozi wa Shirika la Agape kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma shule ya Agape ili kujistili na hedhi.


Na Marco Maduhu - Shinyanga.

Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga kwa kushirikiana na wadau wanaopinga matukio ya ukatili wa kijinsia mkoani Shinyanga, zikiwemo mimba na ndoa za utotoni, wameadhimisha kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Maadhimisho hayo yamefanyika leo Desemba 10, 2020 kwenye shule ya Sekondari ya Agape iliyopo Kata ya Chibe manispaa ya Shinyanga, ambayo inalea Mabinti waliofanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia, wakiwemo waliopewa mimba za utotoni pamoja na kuozeshwa katika umri mdogo na kuachishwa masomo. 

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo mgeni rasmi Afisa Maendeleo wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone, akimwakilisha Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, ameitaka jamii pamoja na wadau hao wa maendeleo, kuunganisha nguvu ya pamoja kutokomeza matukio hayo ya ukatili wa kijinsia. 

Amesema matukio ya ukatili wa kijinsia mkoani Shinyanga, yamekuwa yakitendwa na jamii yenyewe kutokana na kuendekeza mila potofu ambazo zinakandamiza jinsi ya kike, pamoja na kuwaficha watuhumiwa ambao wamekuwa wakifanya matukio hayo, na kumaliza kesi kimya kimya na kusababisha kutofungwa jela. 

“Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia mwaka huu inasema, “tupinge ukatili mabadiliko yana anza na mimi”, hivyo jamii tukibadilika sisi wenyewe kukemea vitendo hivi pamoja na kuungana, matukio haya zikiwamo mimba na ndoa za utotoni zitakwisha kabisa,”amesema Kiwone. 

“Sisi kama Serikali tumekuja leo kuadhimisha kilele cha kupinga siku 16 za matukio ya ukatili wa kijinsia kwenye shule hii ya Agape  ACP, ambayo inalea wahanga wa matukio ya ukatili na kuwapatia elimu ya mfumo usio rasmi, ili kila mmoja aguswe na kupinga vitendo vya ukatili kuanzia ngazi ya familia,”ameongeza. 

Naye Mwanasheria wa Shirika la Agape APC Felix Ngaiza, akizungumza kwenye maadhimisho hayo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Shirika hilo John Myola, amesema Shirika hilo lilianzisha mfumo huo wa kutoa elimu kwa mfumo usiyo rasmi (QT), kwa Wahanga hao wa mimba na ndoa za utotoni ili wapate kutimiza ndoto zao ambazo zilitaka kuzimwa mara baada ya kuachishwa masomo. 

Pia ameishukuru serikali ya mkoa wa Shinyanga kwa kuendelea kushirikiana kikamilifu na Shirika hilo, pamoja na kutatua baadhi ya changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili, na kuwapatia misaada mbalimbali ikiwamo chakula. 

Kwa upande wake Ofisa Maendeleo ya jamii Kata ya Chibe Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Kashinje Shija, awali akisoma taarifa ya halmashauri hiyo amesema katika maadhimisho hayo hawajaja mikono mitupu, ambapo Serikali kwa kushirikiana na wadau wameamua kuungana na kutoa msaada wa chakula, sabuni pamoja na taulo za kike. 

Aidha amewataja wadau ambao wametoa msaada huo kuwa ni Shirika la ICS ambalo limetoa kilo 100 za maharage, Rafiki SDO kilo 50, Musoma Food kilo 50, UDIDA kilo 30, CHIDEP kilo 20, Mr na Mrs Mwigulu kilo 20, YWDL kilo 5 wote hao wametoa maharage pamoja na, Baraza la watoto KKKT Makedonia ambalo limetoa Mchele Kilo 10. 

Ametaja mashirika mengine ni WEADO wametoa sabuni za unga na boksi moja na Taulo za kike, YWCA, Restless Development vijana tunaweza, pamoja na UDIDA ambapo wote hao wametoa msaada wa taulo za kike kwa ajili ya kujistiri na hedhi wanafunzi hao ambao ni Wahanga wa mimba na ndoa za utotoni. 

TAZAMA PICHA HAPA CHINI.
Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Afisa Maendeleo ya jamii manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho hayo kwa niaba ya Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi
Mwanasheria wa Shirika la Agape Felix Ngaiza, akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, akimwakisha Mkurugenzi wa Shirika hilo John Myola. 
Afisa miradi kutoka Shirika la Agape Peter Amani, akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatli wa kijinsia.  
Ofisa maendeleo ya jamii Kata ya Chibe manispaa ya Shinyanga Kashinje Shija, akisoma taarifa kwenye kilele cha maadhimisho hayo ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.Wananchi wakiwa kwenye kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
Wananchi wakiwa kwenye maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
Viongozi mbalimbali kuanzia ngazi ya Kata, Halmashauri, na wadua wakiwa kwenye kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
Maadhimisho ya kilele cha kupinga siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
 

Afisa maendeleo ya jamii halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone (katikati), akikabidhi Taulo za kike kwa viongozi wa Shirika la Agape kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma shule ya Agape ili kujistiri na hedhi.
Misaada ikiendelea kutolewa.
Misaada ikiendelea kutolewa.
Msaada wa chakula ukiendelea kutolewa ikiambatana na picha ya pamoja.
Msaada wa chakula ukiendelea kutolewa pamoja na picha ya pamoja ikipigwa.
Chakula kikiwa katika shule ya Agape. Maandamano ya kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia. Maandamano ya kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia. 
Maandamano yakiendelea.
Maandamano ya kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia

Na Marco Maduhu- Shinyanga. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post