MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI STELLA JOEL AACHIA WIMBO MPYA "TANZANIA YA MAENDELEO"


Mwimbaji wa Muziki wa Injili Nchini Tanzania na Katibu wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Stella Joel akiwa katika muonekano wa picha tofauti baada ya kuachia wimbo wa kuhamasisha maendeleo unaoitwa Tanzania ya Maendeleo.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI


Na Dotto Mwaibale


BAADA ya kimya cha muda mrefu, Mwimbaji wa Muziki wa Injili Nchini Tanzania, Stella Joel ameachia wimbo wa kuhamasisha maendeleo unaoitwa 'Tanzania ya Maendeleo'.

Mara ya mwisho Stella aliachia wimbo wa Hakuna Mwanamke mbaya alioshirikiana na malkia wa muziki wa Injili, Rose Muhando.

Stella ambaye ni Katibu wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) amesema, imefika hatua kwa wasanii kuhamasisha nyimbo zinazochochea maendeleo na kuisaidia jamii kutatua changamoto zake.

“Baada ya Tanzania kufikia uchumi wa kati nikaona ni vyema niweke hilo kwenye muziki, nyimbo za aina hii zinachangia sana kupiga hatua za kimaendeleo zaidi,” amesema Stella.

Stella amewashauri wanamuziki nchini kubadilisha mtizamo wao, kutojikita kwenye  jumbe za mapenzi peke yake badala yake waangalie changamoto nyingi za kijamii kama masuala ya lishe, ukatili wa kijinsia na mengine.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments