MWILI WA MAREHEMU WAPOTEA KWENYE JENEZA KAHAMA

Picha haihusiani na habari hapa chini

Wananchi wa Kijiji cha Kona Nne Wilaya ya Kaliua mkoani wa Tabora wameshangazwa na kurejea kwa mwili wa marehemu aliyefariki dunia kwao na kusafirishwa kwenda Kahama kwa ajili ya mazishi na wakati wakijiandaa kwa mazishi mwili ukarudi kwa mazingira ya tatanishi kijijini hapo.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha King’wangoko Said Nzogola amethibitisha kutokea kwa tukio hilo juzi na kusema kuwa mwili huo umerudi Tabora na kwamba kabla ya kuusafirisha kwenda Kahama ndugu wa marehemu walidai mahari ya binti yao.

“Waliondoka wameubeba na kaka yake kutoka tumbo moja alikuwepo na walipofika kule nao wakashangaa umepotea kwenye jeneza na baadae jioni wakarudi kuchukua mwili tena na mwanzo kabla tukio hilo halijatokea walikuwa wanadai mahari shilingi Mil.1.5,” amesema Said Nzogola.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post