MHUBIRI WA KIMATAIFA DONNA MOLLEY AMPONGEZA RAIS MAGUFULI


Na Grace Mwakasendile Mbeya

 Mhubiri wa Kimataifa wa Injili  kutoka nchini Marekani,  Donna Molley  amempongeza Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John  Poombe Magufuli kwa ujasiri wake wa kupambana na Ugonjwa wa Covid – 19 unaosababishwa na maambukizi ya  Virusi vya Corona  akieleza  kwamba ni kiongozi wa kwanza duniani ambaye amemshikirisha Mungu katika mapambano ya ugonjwa huo.

Mhubiri wa Kimataifa wa Injili  kutoka nchini Marekani,  Donna Molley  ametoa pongezi hizo akiwa mkoani Mbeya baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe, kwa ajili ya kuhubiri kwenye mkutano mkuu wa injili ambayo utafanyika kwa siku 4 mfululizo  kwenye uwanja Ruanda Nzovwe jijini Mbeya.

Amesema  Rais Dk. Magufuli ni mfano wa kuigwa kutokana na utendaji kazi wake pamoja na imani aliyonayo katika kumtegemea Mungu na kushinda katika vita dhidi ya ugonjwa wa Covid 19.

Naye profesa Donald Mwanjoka ambaye ni Mwenyekiti wa Makanisa ya Kipentekoste katika Mkoa wa Mbeya amemtaja  Rais Dk.  Magufuli kuwa ni  kiongozi ambaye anamshirikisha Mungu katika kila hatua za uongozi wake.

Ameahidi yeye na viongozi wengine wa dini kuendelea kumuombea na kumpa ushirikiano katika kila jambo analolifanya ili kuliletea maendeleo taifa la Tanzania.

Mkutano Mkuu wa Injili unatarajiwa   kufanyika kuanzia Desemba 10 hadi 13 ukitanguliwa na kongamano la Wanawake,  ambapo wagonjwa mbalimbali wataombewa wakiwemo wenye mahitaji maalum.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments