WAZIRI MKUU ATOA SIKU 15 KUKAMILIKA KWA HOSPITALI YA UHURU | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, November 21, 2020

WAZIRI MKUU ATOA SIKU 15 KUKAMILIKA KWA HOSPITALI YA UHURU

  Malunde       Saturday, November 21, 2020


Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Mjaliwa (Mb) ametoa siku 15 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) na Suma JKT kuhakikisha ujenzi wa Hospitali ya Uhuru unakamilika ifikapo disemba 5, 2020.

Akikagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali hiyo jana Jijini Dodoma Mhe. Majaliwa amesema Hospitali ya Uhuru ni moja kati ya miradi ya kimkakati ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuimarisha utoaji huduma katika Sekta ya afya ambayo inaanzia kuboresha kuanzia ngazi ya zahanati, vituo vya Afya, Hospitali za Wilaya, Hospitali za Rufaa na Hospitali za Magonjwa makubwa.

Anaendelea kufafanua kuwa Serikali imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha inaboresha huduma za afya kwa lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi, hivyo imejikita katika kuhakikisha miradi yote ya kimakakati inakamilika kwa wakati ili ianze kutumika

“ Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Wakala wa majengo (TBA), Suma JKT, hakikisheni ujenzi wa Hospitali hii unakamilika kwa wakati, fanyeni kazi usiku na mchana, jengeni vibanda na kuhamia kwenye eneo la ujenzi, ongezeni wafanyakazi ili kukamilisha ujenzi kwa wakati uliopangwa” amesisitiza Mhe. Majaliwa

Mhe. Majaliwa amesema miradi ya Kimakakati inatakiwa ikamilike kwa wakati na Watanzania wanahamu ya kuona miradi inakamilika na kuanza kutoa huduma hivyo fanyeni kazi kwa weledi ili kuweza kukamilisha ujenzi wa Hospitali hiyo muhimu kwa jamii

Akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Chamwino, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Joseph Nyamhanga amesema ujenzi wa Hospitali ya Uhuru imekadiriwa kutumia zaidi ya shilingi bilioni 3.995 na kiasi kilichotengwa ni shilingi bilioni 3.410 ambapo zaidi ya shilingi milioni 995 zilikuwa ni fedha za maadhimisho ya siku ya uhuru wa Tanganyika na shilingi bilioni 2.415 ni gawio la kampuni ya simu ya Airtel.

Naye Msaidizi wa Mkuu wa JKT Colonel Laurence Angelo Lupenge amesema mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Uhuru umefikia asilimia 92 na kazi zilizofanyika ni kusafisha eneo la mradi,kuchimba na kujenga msingi, kujenga “frame” ya jengo pamoja na kuta, kupiga “plaster” kuta pamoja na” skimming”, kuweka njia za mifumo ya umeme,kupaua na kufunga gypsum board,kuchimba mashimo ya maji taka na kuweka “rough floor” kwa ajili ya kuweka vigae
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post