VIONGOZI WA CHADEMA WAKAMATWA KWA KURATIBU MAANDAMANO

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, ACP Lazaro Mambosasa amesema wanawashikilia watu kadhaa wakiwemo viongozi  wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa tuhuma za kupanga maandamano.

Viongozi wa Chadema wanaowashikilia ni pamoja na mwenyekiti wa chama hicho taifa, Freeman Mbowe, Godbless Lema, na Boniface Jacob aliyekuwa Meya wa Ubungo na mgombea ubunge wa Jimbo la Ubungo.

Amesema wanawashikilia viongozi hao kwa kuwa wanahatarisha usalama wa raia na mali zao kwa kuwa wamepanga kuanza maandamano kitaifa yasiyokuwa na kikomo

Aidha, jeshi hilo linaendelea kuwasaka watu wanaowashawishi vijana kushiriki maandamano ambayo polisi wamesema ni ya vurugu. Wengine wanaosakwa ni viongozi wa chama cha ACT Wazalendo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments