RC SHIGELLA APIGA MARUFUKU MAANDAMANO NA MIKUSANYIKO

MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza 
madereva wa pikipiki maarufu bodaboda waliokusanyika kwa ajili ya kumpongeza Rais Dkt John Magufuli kwa kuchaguliwa tena kuongoza Tanzania kwa kipindi kingine cha miaka mitano kushoto Katibu wa kikundi cha Tanga One cha wilaya ya Tanga  Omari Ahmed
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza 
madereva wa pikipiki maarufu bodaboda waliokusanyika kwa ajili ya kumpongeza Rais Dkt John Magufuli kwa kuchaguliwa tena kuongoza Tanzania kwa kipindi kingine cha miaka mitano kushoto Katibu wa kikundi cha Tanga One cha wilaya ya Tanga  Omari Ahmed
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akiteta jamboi na viongozi waendesha pilkipiki bodaboda Jijini Tanga cha Tanga One wakati akipokea maandamano yao waliokusanyika uwanja wa Lamore kwa ajili ya kumpongeza Rais Dkt John Magufuli kwa kupata ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika Octoba 28 mwaka huu
KATIBU Mwenezi wa CCM wilaya ya Tanga Lupakisyo Kapange akizungumza 


MKUU wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella amepiga marufuku aina yoyote ya maandamano na mikusanyiko huku akiwataka wananchi kuendelea kujikita kwenye shughuli za kimaendeleo kwa maslahi mapana ya Taifa kutokana na kwamba uchaguzi umekwisha na walioshindwa wakubali matokeo.

RC Shigella aliyasema hayo wakati madereva wa pikipiki maarufu bodaboda waliokusanyika kwa ajili ya kumpongeza Rais Dkt John Magufuli kwa kuchaguliwa tena kuongoza Tanzania kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Alisema kwamba amepokea maandamano hayo ili atumie nafasi hiyo kuwatangazia wananchi kwamba serikali hairuhusu mikusanyiko yoyote katika kipindi hiki ambacho uchaguzi umemalizika.

Hatua ya Mkuu huyo wa Mkoa kupiga marufuku maandamano au mikusanyiko yoyote imekuja kutokana na uwepo wa tetesi kwamba wafuasi wa baadhi ya vyama vya upinzani wanaandaa maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi huo.

Awali akisoma risala ya umoja wa waendesha bodaboda kikundi cha Tanga One cha wilaya ya Tanga iliyosomwa na Katibu wao Omari Ahmed alisema wanampongeza Rais Dkt John Magufuli kwa ushindi walioupata na kwamba wana matumaini kwamba sasa wana uhakika wa kufanya kazi zao kwa utulivu.

Alisema wanampongeza kwa dhati Rais Magufuli kwa kuibuka na ushindi wa kishindo kwani walikuwa wanamuombea kila wakati katika mchakato huo wa kuwania nafasi hiyo.

“Lakini tunapongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuhakikisha amani ya Taigfa inakuwa shwari wakati wote huu wa uchaguzi na umekwisha sasa tunaangalia maendeleo zaidi na kauli mbiu ya Rais Dkt Magufuli hapa kazi tu”Alisema

Hata hivyo alisema wao bodaboda kwa niaba ya wenzao wanaombi kwa Rais wanaomba aendelee kuwakumbuka watu wa Tanga huku wakiomba wakati akiapishwa waalikwe watu 10 wa bodaboda waende kushuhudia tukio hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments