RAIS MTEULE WA MAREKANI JOE BIDEN ATANGAZA KUUNDA JOPO LA WATAALAM KUHUSU COVID-19


Jopo hili la "wataalam mashuhuri" litateuliwa kuanzia Jumatatu na litatakiwa kuanzisha mpango wa utendaji kuanzia Januari 20, 2021, siku ya kuapishwa kwa rais mpya.

Joe Biden amekua akilitaja jopo hili kila mara katika hotuba yake: vita dhidi ya janga la Covid-19, ambalo limeua watu 237,000 nchini Marekani itakuwa kipaumbele chake cha kwanza. 

Kwa kufanya hivyo, Joe Biden ametangaza kwamba ataanzisha kitengo cha kukabiliana na ugonjwa huo hatari kuanzia Jumatatu, Novemba 9, akiwaleta pamoja "wanasayansi mashuhuri na wataalam" kupambana na changamoto kuu inayoikabili sasa serikali ya Marekani.

"Jumatatu, nitaanzisha, nitateuwa jopo la wanasayansi na wataalam" kufanya kazi "juu ya mpango ambao utaanza kutumika mnamo Januari 20, 2021", siku ya kuapishwa kwangu, amesema rais mteule mbele ya umati wa wafuasi wake waliokusanyika huko Wilmington, Delaware kusherehekea ushindi wake.

Katika wiki hii ya uchaguzi wa urais, Marekani imerekodi idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya Corona kutokana na mlipuko mpya wa janaga hilo kwa siku kadhaa. Marekani ilirekodi zaidi ya visa vipya 122,000 vya maambukizi ya virusi vya Corona siku ya Jumamosi kwa muda wa saa 24, kulingana na takwimu za shirika la habari la AFP




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments