MSEMAJI MKUU WA SERIKALI DKT. HASSAN ABBASI APANGUA HOJA ZA WAPINZANI | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, November 10, 2020

MSEMAJI MKUU WA SERIKALI DKT. HASSAN ABBASI APANGUA HOJA ZA WAPINZANI

  Malunde       Tuesday, November 10, 2020


 MSEMAJI Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Dkt. Hassan Abbasi ameliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kuwa Watanzania wamemaliza uchaguzi na sasa wanaendelea na michakato ya kidemokrasia, kisheria na kikatiba ya kujenga taasisi za nchi ili kazi iendelee na kamwe hawapotezi muda na kile alichokiita “maigizo” ya baadhi ya viongozi wa upinzani hasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

“Hivi ninavyoongea na wewe mchakato unaofuata ni bunge kuanza, watachagua spika, watapelekewa jina la waziri mkuu kumthibitisha na kisha rais atazindua bunge, hao walioshindwa uchaguzi na kuanza tuhuma ni maigizo yao ambayo tumeyazoea kila mara wanaposhindwa,” amesema.

Akijibu  madai ya baadhi ya viongozi wa Chadema kuhofia usalama wao na hata kujaribu kuomba hifadhi ya ukimbizi nje ya nchi  Abbasi alishangazwa na madai hayo na kuhoji wametishiwa usalama wao na nani, wapi na lini?

“Mkataba wa Kimataifa wa Mwaka 1951 unaohusu Haki na Hadhi za Wakimbizi kwa mfano unaainisha bayana taratibu za kuwa mkimbizi, huwezi kuamka asubuhi tu ukajitangaza wewe ni mkimbizi au una kesi ya jinai ukataka kukimbia nchi kisa kudai ukimbizi.

“Mtu anaibuka anadai ametishiwa maisha lakini juzi tu katoka kushiriki kampeni siku 60 na amelindwa salama kabisa leo kashindwa anakwambia anahofia maisha. Mkimbizi gani anavuka mpaka mbele kaandaliwa gari ya kumchukua? Haya ni maigizo,” alisema.

Amesisitiza kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kuenzi misingi ya amani na kuwataka Watanzania kuendelea kuchapa kazi, anayehofu usalama wake atoe taarifa kwenye vyombo vya dola 

==>>Msikilize hapo chiniUsikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post