MKURUGENZI RASILIMALI WATU TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI AWANOA WATUMISHI | MALUNDE 1 BLOG

Friday, November 13, 2020

MKURUGENZI RASILIMALI WATU TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI AWANOA WATUMISHI

  TANGA RAHA BLOG       Friday, November 13, 2020

 

Mkurugenzi wa Rasilimali watu kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bi Mary Mwangisa, akitoa maelekezo wa baadhi ya watalaam watakaoshiriki katika elimu ya mafunzo na matunzo ya miondombinu ya umwagiliaji kwa wakulima.
Mkurugenzi msaidizi wa idara ya mafunzo na matunzo kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Enterbert Nyoni akifafanua jambo wakati wa kikao na wataalam,cha maandalizi ya utoaji elimu kwa wakulima kuhusiana na utunzaji wa miundominu ya Umwagiliaji.kulia, ni Bw.Reginald  Diamett Meneja Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo cha Umwagiliaji.

Picha ikionesha sehemu ya washiriki katika kikao hicho cha maandalizi.


 Na MwandishiWetu Dodoma

Mkurugenzi Rasimali watu kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bi. Mary Mwangisa,  amewapa maekelezo baadhi ya watumishi wa ofisi hiyo watakaoshiriki katika zoezi la utoaji elimu na mafunzo ya utunzaji wa miundombinu ya kilimo cha umwagiliji katika baadhi ya skimu za kilimo hicho nchini.

Akikaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo, Bi Mwangisa amesema kuwa  watumishi hao wanapaswa kuzingatia mwongozo wa namna ya kutoa mafunzo ya vyama vya umwagiliaji wa namna ya kukusanya mapato kwa ajili ya uchangiaji wa mfuko wa maendeleo ya umwagiliaji, matumizi sahihi ya kalenda za kilimo na utunzaji wa miundombinu ya umwagiaji.

“Serikali imewekeza pesa nyingi katika miundombinu ya umwagiliaji kwa hiyo  isipotunzwa serikali itapata hasara, na wakulima wataathirika, vyama vya umwagiliaji vitakufa na miundombinu hiyo itakufa.” Alisisitiza.

Aliendelea kusema kuwa kilimo cha umwagiliaji ni moja kati ya mategemeo ya kuongeza uzalishajiwa mazao ya chakula na biashara na uhakika wa usalama wa chakula nchini.

Maelekezo hayo kwa watumishi yametolewa ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mkakati wa tume ya taifa ya umwagiliajiwa kutoa elimu kwa vyama vya umwagiliaji nchini.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post