DKT MATARAGIO: TPDC TUMEYATUMIA MASHINDANO YA SHIMUTA KUJITANGAZA YAMEKUWA NA TIJA KUBWA

 MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) Dkt James Mataragio  akizungumza na wachezaji wa timu za shirika hilo ambazo zinashiriki kwenye michuano ya Shimuta inayoendelea kutimua vumbi kwenye viwanja mbalimbali mjini hapa.

MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) Dkt James Mataragio  kulia akiwa na Katibu wa Michezo wa Shirika hilo Elinaike Naburi wakiwasikiliza watumishi wa shirika hilo ambao ni wanamichezo wanaoshiriki mashindano ya Shimuta Jijini Tanga
Mmoja wa wachezaji wa timu ya TPDC akichangia jambo wakati wa kikao hicho na Mkurugenzi wa TPDC Dkt James Mataragio ambaye hayupo pichani
Mmoja wa wachezaji wa timu ya TPDC akichangia jambo wakati wa kikao hicho na Mkurugenzi wa TPDC Dkt James Mataragio ambaye hayupo pichani
Sehemu ya watumishi wa TPDC ambao wanashiriki mashindano ya Shimuta Jijini Tanga wakimsikiliza Mkurugenzi wa Shirika hilo Dkt James Mataragio
Sehemu ya watumishi wa TPDC ambao wanashiriki mashindano ya Shimuta Jijini Tanga wakimsikiliza Mkurugenzi wa Shirika hilo Dkt James Mataragio
Mkurugenzi wa Shirika hilo Dkt James Mataragio  wa pili kutoka kushoto akiwa kwenye picha ua pamoja na wachezaji wa timu za shirika hilo ambazo zinashiriki mashindano ya Shimuta

MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) Dkt James Mataragio amesema wameyatumia mashindano ya Shimuta yanayoendelea Jijini Tanga kama njia ya kujitangaza hivyo yatakuwa na tija kwao kutokana na kwamba wamekuwa wakifanya biashara ya kuuza gesi na shughuli za kutafuta mafuta.

Dkt Mataragio aliyasema hayo leo jijini Tanga wakati akizungumza na wachezaji wa timu za shirika hilo ambazo zinashiriki kwenye michuano ya Shimuta inayoendelea kutimua vumbi kwenye viwanja mbalimbali mjini hapa.

Mkurugenzi huyo ambaye alifika Jijini Tanga leo asubuhi kushiriki katika timu yao inayoshiriki kwenye mashindano ya Shimuta amesema wamekuwa washiriki wazuri kwa miaka mingi.

Alisema kila siku Shirika hilo limekuwa na timu ya ushindi ambapo wamekuwa wakifanya hivyo katika mashindano mbalimbali huku akieleza mwaka huu wamekuwa mahiri kwa kuweza kuleta ushindani.

Aidha alisema umahiri huo umesaidia kuleta ushindani kwenye michezo mbalimbali kwa mfano mchezo wa Wavu,Kikapu,Riadhaa,Karata ,Pete na Mpira wa Miguu ambapo wameshiriki kote na kuweza kushinda vikombe sita na kupata medali moja lakini kikubwa zaidi wamejenga afya ya wafanyakazi wao.

“Ushiriki wetu umekuwa na umuhimu kwa sababu michezo ni afya na inaongeza tija kwa hiyo mimi kama Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC nalitambua hilo na ndio maana siku zote nawatia moyo vijana wetu kushiriki kwenye michezo kwa sababu najua michezo inaleta tija”Alisema

“Lakini kikubwa zaidi sisi kama TPDC ni shirika la Serikali ambalo linafanya biashara ya kuuza gesi na shughuli za kutafuta mafuta hivyo kushiriki kwenye michezo hiyo ni kuitangaza TPDC na shughuli ambazo tunazifanya “Alisema

Alisema kwa sababu wanatumia fedha nyingi kujitangaza lakini kwa vijana wao kushiriki kwenye michezo hiyo wanatangaza bidhaa zao kwa namna moja au nyengine kwa sababu wana kukutana na watu wengi kutokana na michezo huusisha watu wengi na wanajitangaza na kufahamika wanafanya nini na ni nani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post