DC KOROGWE AWAHIMZA MADEREVA BODABODA KUJIUNGA NA MPANGO WA BIMA YA AFYA

 

_MG_9466MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa akizungumza na madereva wa waendesha pikipiki za magurudumu mawili na matatu wilayani humo kuhusu umuhimu wa kujiunga na mpango wa bima ya afya wakati wa uzinduzi wa mpango huo kwao kushoto ni Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu na kulia ni Mkuu wa Usalama Barabarani wilaya ya Korogwe (DTO) Leonard Bandola


_MG_9323
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kulia akizungumza wakati wa uzinduzi huo


_MG_9380
Mkuu wa Usalama Barabarani wilaya ya Korogwe (DTO) Leonard Bandola akizungumza wakati wa uzinduzi huo


_MG_9358
AFISA Matekelezo wa NHIF Mkoa wa Tanga Macrina Clemence akisisitiza jambo


_MG_9381
Mwenyekiti wa Waendesha pikipiki za magudumu mawili na matatu wilayani Korogwe Mohamed Kombo Kapaya akitoa ushuhuda kwa wenzake namna bima ya afya ilivyomsaidia


_MG_9267
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kulia akitoa elimu kwa mwendesha pikipiki za magurudumu matatu kabla ya kuanza ufunguzi wa mpango wa elimu ya bima ya afya kwao katikati ni Mkuu wa Usalama Barabarani wilaya ya Korogwe (DTO) Leonard Bandola

_MG_9276
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kulia akitoa elimu kwa mwendesha pikipiki za magurudumu matatu kabla ya kuanza ufunguzi wa mpango wa elimu ya bima ya afya kwao kushoto ni Mkuu wa Usalama Barabarani wilaya ya Korogwe (DTO) Leonard Bandola
_MG_9336

WAENDESHA Pikipiki za magurudumu mawili na matatu wilayani Korogwe mkoani Tanga wamehimizwa kuchangamkia fursa ya kujiunga na mpango wa bima ya afya ili waweze kuwa na uhakika wa matibabu wanapokuwa wakiugua.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa wakati akizindua mpango wa Bima kwa madereva wa pikipiki za magurudumu mawili na matatu wilayani Korogwe uliofanyika kwenye uwanja wa Mazoezi.

Alisema bima ya afya ndio silaha pekee ambavyo inaweza kuwahakikishia uhakika wa matibabu wakati wanapoumwa huku wakiwa hawana fedha hivyo ni muhimu kuichangamkia na kujiunga nayo .

“Ndugu zangu maradhi huja bila kutegemea hivyo niwasihi mhakikishe mnachangamkia fursa hii ya kujiunga na mpango wa bima kwani ni mkombozi mkubwa sana na utakuwa na uhakika wa matibabu “Alisema

Aidha alisema lakini gharama za matibabu zimekuwa zikipanda kila siku hivyo iwapo watajiunga na mpango huo wa bima utawasaidia kuwapunguzia gharama za kupata matibabu.

Awali akizungumza wakati wa uzinduzi huo,Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu alisema lengo la kukutana na makundi hayo ni kuweza kuwahamasisha wajiunga na mpango wa bima ya afya ambao ni muhimu kwa maisha yao na unawahakikishia uhakika wa matibabu.

Alisema makundi hayo ni moja ya watu ambao wanakabiliwa na changamoto za ajali wanapokuwa kwenye shughuli zao hivyo kujiunga na mpango wa bima atawawezesha kupata huduma za matibabu pindi watakapoungua.

Alisema kwamba wanaweza kulipa kwa awamu kwa utaratibu wa kupitia kwa uongozi wao unaweza kuzipeleka kwenye kupitia benki ya NMB ili wawezesha kunufaika na huduma za matibabu badala ya kufikiria kupata fedha tunakwenda kufanyia mambo mengine.

“Ndugu zangu hakuna anayejua ugonjwa utaingia muda gani au siku gani hivyo ni muhimu kuhakikisha tunajiunga na bima ya afya kwa lengo la kuwa na uhakika wa matibabu pindi na hii itawasaidia kuepuka kutumia gharama kubwa za matibabu”Alisema Mwakababu.

Naye kwa upande wake Mwenyekiti wa Waendesha Pikipiki za magurudumu mawili na matatu wilayani Korogwe mkoani Tanga Mohamed Kombo Kapaya aliwashukuru mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) kwa kuwakumbuka wao madereva wa kuwaingia kwenye mfumo wa matibabu kwa gharama nafuu.

Alisema kwamba umuhimu wa kuwa na bima ya afya ni mkubwa huku akitolea historia yake mwenyewe wakati alipopata tatizo la kuugua mwaka 2011-2012 tukio ambalo lilisababisha kutoka kuhamishwa kwenye Hospitali ya wilaya ya Korogwe na kuhamishiwa KCMC.

Mwenyekiti huyo alisema wakati huo alikuwa akifikiria angewezeje kulipa gharama za matibabu lakini kwa kuwa mke wake ni mwalimu alimkatia bima na hivyo kumsaidia katika matibabu yake ambapo alifanyiwa upasuaji KCMC na huduma nyengine muhimu.

“Hivyo nieleza kwamba kuna umuhimu mkubwa sana kuwa na bima ya afya naomba leo hii kila mtu ajiandikisha na kujiunga kwenye mpango huu “Alisema

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments