BIDEN APATA MAFANIKIO YATAKAYOMWEZESHA KUSHINDA KITI CHA RAIS WA MAREKANI | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, November 5, 2020

BIDEN APATA MAFANIKIO YATAKAYOMWEZESHA KUSHINDA KITI CHA RAIS WA MAREKANI

  Malunde       Thursday, November 5, 2020


Mgombea wa kiti cha urais kupitia chama cha Democratic nchini Marekani, Joe Biden amepiga hatua muhimu kuelekea kupata ushindi baada ya kunyakua majimbo tete ya Michigan na Wisconsin usiku wa kuamkia leo.

 Katika taarifa fupi aliyoitoa akiwa pamoja na mgombea mwenza Harris Kamala, Biden amesema hawezi kujitangazia ushindi lakini ana matumaini kuwa zoezi la kuhesabu kura litakapomalizika wataibuka kuwa washindi. 

Kwa kunyakua majimbo hayo mawili, Biden amefikisha kura 264 za Baraza maalumu la wajumbe wanaomchagua rais dhidi ya 214 za rais Doanld Trump anayewania muhula wa pili.

 Trump amezungumzia mafanikio hayo ya Biden kwa hasira na tayari amewasilisha ombi la kufungua shauri dhidi ya matokeo hayo ikiwa ni pamoja na kutaka kura kuhesabiwa tena na katika baadhi ya majimbo ametaka zoezi la kuhesabu kura kusitishwa.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post