RAIS DKT MAGUFULI AMUANDIKIA BARUA KIONGOZI MPYA WA KUWAIT

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amwandikia barua ya salamu za rambi rambi Kiongozi mpya (Amir) wa Kuwait,Mtukufu Sheikh Nawaf Al-Ahmad Al-Sabah kufuatia kifo cha aliyekuwa kiongozi wa Taifa hilo Mtukufu Sheikh Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-sabah.

Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi wa Kuwait hapa nchini amemkabidhi Balozi wa Kuwait Mhe.Mubarak Mohammed Alsehaijan barua iliyoandikwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwenda kwa Kiongozi mpya wa Kuwait.

Prof. Kabudi amesema Tanzania na Kuwait zina mahusiano mazuri sana na muda mrefu katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo akitolea mfano wa mfuko wa Kuwait ambao umekuwa wa msaada mkubwa katika kwa Tanzania ambao umekuwa ukisaidia katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali hapa nchini ikiwemo barabara.

Ameongeza kuwa msiba wa Kiongozi huyo wa Kuwait ni msiba wa Watanzania wote kwa kuwa kwa muda wote ambao Hayati Sheikh Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-sabah amekuwa Kiongozi wa Taifa hilo amekuwa karibu sana na Tanzania.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527