NEC YAVITAHADHARISHA VYAMA VYA SIASA NA WAGOMBEA KUHUSU UVUNJIFU WA SHERIA ZA NCHI


Na Allawi Kaboyo – Bukoba.

Wakati vyama vya siasa nchini vikiendelea na zoezi la kuomba kuchaguliwa na wananchi kushika nafasi mbalimbali za uongozi, Tume ya uchaguzi NEC ivitahadharisha vyama hivyo kutofunja dheria za nchi kwa kigezo cha uchaguzi.

Katika hotuba ya mwenyekiti  wa NEC iliyosomwa na mkurugenzi wa mipango, ufatiliaji na tathmini wa tume ya  Taifa ya uchaguzi  Adam Mkina wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoani Kagera uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa RAS Kagera Oktoba 05, mwaka huu, ameeleza kuwa pamoja na masuala yote ya uchaguzi suala la utulivu na amani vinatakiwa kupewa kipaumbele.

Amesema kuwa Tume imekuwa ikisisitiza umuhimu wa vyama vya siasa na wagombea kuzingatia maadili ya uchaguzi katika kampeini zao, ikiwemo kuepuka lugha za kashfa maneno ya uchochezi yanayotishia amani na usalama wa nchi pamoja na kuhakikisha wanaepuka kufanya kampeini ambazo zinaashiria ubaguzi katika  misingi ya jinsia, ulemavu, ukabila, udini, maumbile au Rangi.

“Tunaendelea kuwasisitiza vyama na wagombea kuwa kunapokuwa na malalamiko yoyote ya kimaadili basi hatua stahiki zichukuliwe ikiwemo,kuwasilisha malalamiko kwenye kamati za maadili ndani ya muda uliyowekwa na sio kwenye vyombo vya habari au mitandao ya kijamii.” Amesisitiza Adam

Mkina ameongeza kuwa tume inaendelea kuratibu  kusimamia na kuendesha uchaguzi huu kwa kutumia sheria za uchaguzi, ambapo amesisitiza kuwa vyama vya siasa wagombea na wananchi wanakumbushwa kuwa katika kipindi hiki, sheria nyingine za nchi hazijasimama hivyo wajihadhari na vitendo ama mattamshi ambayo yanaweza sababisha vurugu kwa kisingizio cha uchaguzi.

Aidha ameongeza kuwa katika uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura umewezesha daftari hilo kuwa na jumla ya wapiga kura 29,188,347 nchi  nzima, ambapo pia wagombea kutoka vyama vya siasa 15 waliteuliwa na kugombea nafasi za urais huku wawili kati yao wakiwa wanawake pamoja na wanawake 5 kuteuliwa kuwa wagombea wenza.

Kwa upandewake Msimamizi wa uchaguzi manispaa ya Bukoba ambaye ni mkurugenzi wa halmashauri hiyo amewahakikishia wananchi wa manispaa hiyo kuwa uchaguzi utakuwa wa huru na haki hivyo wanao wajibu wa kujiokeza kupiga kura kwaajili ya viongozi wanaowataka.

Mkutano huo umewakutanisha wadau ambao ni waandishi wa habari, vongozi wa dini, asasi za kiraia, watu wenye ulemavu na mashirika mbalimbali yanayojihusisha na elimu ya mpiga kura.


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527