MGOMBEA AAHIDI WANANCHI KATA YA MAGADU MKOANI MOROGORO KUNUFAIKA NA UWEPO WA CHUO CHA SUA



Mgombea Ubunge Viti Maalumu Mkoa wa Morogoro, Dkt. Christine Ishengoma akizungumza kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni Kata ya Magadu Manispaa ya Morogoro.
Wananchi wa Kata ya Magadu na viunga vyake wakisikiliza Sera na ahadi za viongozi na Mgombea wa CCM kata ya Magadu.
Wananchi wa Kata ya Magadu na viunga vyake wakisikiliza Sera na ahadi za viongozi na Mgombea wa CCM kata ya Magadu.
 Mtia Nia Jimbo la Morogoro Mjini Bwana Salumu Mkolwe akizungumza kwenye  mkutano huo wa ufunguzi wa Kampeni kata ya Magadu.
Mwwnyekiti wa UWT Wilaya ya Morogoro Bi.  Victoria  Saduka akizungumza na wananchi wa Magadu wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo.
Katibu wa UVCCM Wilaya ya Morogoro Manispaa bwana Hussein Egobano ambaye ndiye Mgeni rasmi kwenye mkutano huo wa ufunguzi wa Kampeni za Udiwani kata ya Magadu akiongea na watu waliofurika kusikiliza Sera za CCM.

 Mgombea Udiwani Kata ya Magadu kwa TIketi ya CCM bwana Kiduka Juma Issa akijinadi mbele ya wananchi wa Magadu wakati wa uzinduzi huo wa Kampeni za Udiwani kwenye kata hiyo.


Wananchi wa Kata ya Magadu na viunga vyake wakisikiliza Sera na ahadi za viongozi na Mgombea wa CCM kata ya Magadu.


Wananchi wa Kata ya Magadu na viunga vyake wakisikiliza Sera na ahadi za viongozi na Mgombea wa CCM Kata ya Magadu.



Na  Calvin Edward Gwabara -Morogoro.

MGOMBEA  Udiwani kata ya Magadu kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Kiduka Juma Issa amesema akipewa ridhaa kuwa muwakilishi wa wananchi wa kata hiyo atahakikisha anaiunganisha jamii hiyo na Chuo Kikuu Cha Sokoine cha Kilimo SUA ili 
kufaidi mambo makubwa yanayofanywa na watafiti wa Chuo hicho Barani Afrika.

Kiduka aliyasema hayo jana wakati wa Uzinduzi wa Kampeni za Udiwani zilizofanyika kwwnye Mtaa wa Kididimo na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa kata hiyo ambayo imepata bahati ya kuwa na Chuo Kikuu Cha Sokoine cha Kilimo ambacho kinatoa mchango mkubwa kwa Taifa kwenye masuala ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

“Kata yetu ina bahati ya kuzungukwa na wasomi wa SUA nitaunda Tume ya watu 7 ambao watakuwa wananishauri njia na mbinu njema za namna ya kata yetu kukutumia chuo kikuu hiki ili wana Magadu tuwe wa kwanza kuvuna na kunufaika na uwepo wa Chuo hiki cha pekeee nchini kwenye kata yetu” alisema Kiduka.

Akizungumzia miradi mbalimbali ya maendeleo hasa changamoto ya maji kwenye kata ya Magadu Mgombea huyo amesema tayari Serikali ya Magufuli imeshatoka fedha kwa ajili ya kujenga miundombinu ya maji ambayo tayari imeshaanza kujengwa na kwamba kukamilika kwake kutatua kero ya maji kabisa kwenye kata hiyo.

“ Naomba Mnitume kwenye Baraza la madiwani la Manispaa ya Morogoro nikawatumikie tuhakikishe za habari yetu ya kata ya Magadu ina öre she’s na kuanza kutoa huduma za kujifungua kwa wakina mama zetu ambao wanalazimika kwenda Hospitali ya Mkoa na hospitali zingine kwa sasa, sitaki uheshimiwa nataka niwe mtumishi wa kweli” alisisitiza Kiduka.

Pia ametumia nafasi hiyo kuomba kura kwa Mbunge,  Abdulaziz Mohamed Abood na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kwa kusema kuwa Oktoba 28 wachague mafiga matatu yaani Rais, Mbunge na Diwani kutoka CCM 
wasijeweka mafiga mawili ya mawe na figa moja la udongo ambalo muda wowote linaweza kuangusha chungu.

Kwa upande wake Mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa kampeni hizo za Udiwani Kata ya Magadu, Hussein Egobano ambaye ni Katibu wa Umoja wa Vijana wa (UVCCM)  Wilaya ya Morogoro Mjini amesema amewataka wakazi wa Kata ya Magadu wasifanye majaribio kama ambayo zilifanya kata mbili kwenye Manispaa ya Morogoro kwa kuchagua upinzani maana miaka mitano yote hakuna walichokifanya.

Alisema Kata ya Magadu wenyeviti wake wa mitaa  wote wanatoka CCM na Diwani ndiye Mwnyekiti wa Baraza la Maendeleo ya Kata (BMK) hivyo wakichagua diwani wa upinzani watashindwa kuleta maendeleo maana wataishia kulumbana mambo ya siasa wakati wananchi wanataka maendeleo na hivyo kuwataka wamchague Kiduka mgombea wa CCM awe Diwani wao walete maendeleo kwa haraka.

“Lakini pia ndugu zangu wa Magadu naleta salamu nyingi kutoka kwa Mgombea Ubunge wetu  Abood amefanya mambo makubwa ukitaka kujua yote angalia kitabu cha kazi alizofanya katika kipindi cha miaka mitano yeye alikataa kuchukua hela za gari kujinunulia gari akaamua kuzinunulia gari la wagongwa (Ambulence) na sasa sote tunalitumia na magari mengine yanakuja tumeogopa kuyaleta maana watasema anatoa rushwa ila akimaliza kuapishwa tu yatatoka” alisema Egobano.

Aliongeza kuwa “ Tumpe kura za kishindo Rais Dkt. John  Magufuli maana amefanya mambo mengi kwenye Taifa letu na Manispaa ya Morogoro nyinyi ni mashahidi angalieni Soko kubwa la Kisasa, Stand ya Mabasi ya Msamvu, Stendi ya Mabasi madogo ya kisasa na barabara za lami na mambo mengine mengi kwenye maji na afya, ili kumshukuru na kumtia moyo tumwagie kura za kishindo tarehe 28 Oktoba.

Awali Mgombea Ubunge viti Maalumu Dkt. Christine Ishengoma ambaye alikuwepo kwenye uzinduzi huo amewataka wakina mama waache kudanganywa na wapinzani kuwa watawapatia mikopo na kuchukua vitambulisho vyao vya Kupigia kura maana itawanyima haki yao ya msingi ya kupiga kura na mwisho wa siku Wagombea wa CCM wanaowataka watakosa kura zao.

“ Angalieni kazi kubwa iliyofanywa na Mhe. John Pombe Magufuli nchi nzima, niwaombe tujitokeze kwa wingi kupiga kura kuchagua wagombea wa CCM kwenye Udiwani, Ubunge na Urais kwa kishindo ili kata ya Magadu ndio iongoze Kitaifa kwa 

kuchagua kwa kura nyingi CCM na wagombea wake” alisema Ishengoma.

Kwa upande wake akitoa salamu kwa niaba ya Watia nia wa Ubunge Jimbo la Morogoro Mjini na Mwenyekiti wa UVCCM Mstaafu, Salumu Mkolwe alisema Kata ya Magadu imepata bahati sana ya kuwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo na ni fursa kubwa kiuchumi hasa kupitia walimu na wanafunzi wanasoma kwenye Chuo hicho.

“ Kuna miradi mikubwa inatekelezwa na Rais John Magufuli kwenye chuo chetu cha SUA na miradi hii inaongeza idadi ya wanafunzi wanao jiunga na chuo hiki hivyo kuongezeka huko kwa wanafunzi jamii ya Magadu inanufaika kwa kuwapatia huduma mbalimbali za vyakula, malazi na mahitaji mengine na ukiangalia wazee wetu huko mtaani kila mtu nyumbani kwake kapangisha wanafunzi na hao wanafunzi wanalipa kodi Magadu inanufaika” alisisitiza Mkolwe.

Uzinduzi huo wa kampeni kwa kata ya Magadu umeanza jana kwenye mtaa wa Kididimo na kutakuwa na mikutano mingine sita kwenye kila mtaa pamoja na kampeni za nyumba kwa nyumba kwa mujibu wa Mratibu wa Kampeni kata hiyo, Profesa, Mombo ambaye alikuwa Mgombea Ubunge Viti maalumu Mkoani hapa.





Dotto Mwaibale

dotomwaibale@gmail.com
Edit contact

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527