MAWAKALA VYAMA VYA SIASA SHINYANGA MJINI WAAPISHWA

Afisa usimamizi wa uchaguzi mkuu Jimbo la Shinyanga mjini Charles Kafutila, akitoa maelekezo kwa Mawakala wa vyama mbalimbali vya siasa namna ya kujaza fomu za kutunza siri. Picha na Marco Maduhu

Msimamizi wa uchaguzi mkuu Jimbo la Shinyanga mjini Geofrey Mwagulumbi, akitoa maelekezo kwa Mawakala wa vyama mbalimbali vya siasa, wakati wa zoezi la kula kiapo cha kutunza siri.
Mawakala wakijaza fomu kabla ya kula kiapo cha kutunza siri.
Mawakala wakila kiapo cha kutunza siri.

Na Marco Maduhu - Shinyanga
Mawakala wa vyama mbalimbali vya siasa ambao watasimamia zoezi la uchaguzi mkuu katika jimbo la Shinyanga mjini kuwakilisha wagombea wa vyama vyao, wameapishwa na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo Geofrey Mwangulumbi, na kutakiwa kutii sheria na kanuni za uchaguzi ili kuepuka kusababisha vurugu zitakazo vunja amani ya nchi.

Zoezi la kuapisha mawakala hao limefanyika leo, kwenye ukumbi wa mikutano katika kituo cha kulea watoto wenye Ualbino kilichopo Buhangija manispaa ya Shinyanga. 

Mwangulumbi akizungumza mara baada ya kumaliza kuwaapisha Mawakala hao, alisema kila chama kina haki ya kuweka Mawakala, ambao wanapaswa kutii sheria na kanuni za uchaguzi, na wasiwe chanzo cha uvunjifu wa amani kwenye uchaguzi huo. 

“Nawaomba mawakala wa vyama mbalimbali vya siasa ambao mtasimamia zoezi zima la uchaguzi mkuu wakati wa upigaji kura na kuhesabu matokeo mzingatie wajibu wenu pamoja na kufuata sheria na kanuni za uchaguzi, ili ufanyike huru na haki na msiwe chanzo cha kuvuruga amani ya nchi,” alisema Mwangulumbi. 

Nao baadhi ya Mawakala ambao wameapishwa akiwamo Bundala Machiya, walisema watasimamia zoezi hilo kwa kufuata sheria za uchaguzi, ili ufanyike huru na haki na kumalizika salama bila ya kutokea vurugu zozote zile.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments