HAYA NDIYO MAJENGO 10 YENYE THAMANI KUBWA ZAIDI DUNIANI


Utafiti uliofanywa na kampuni ya MSN Money inayohusika na mikataba ya usafirishaji wa pesa, hisa na biashara ya nyumba za makazi duniani imefichua orodha ya majengo yenye gharama ya juu zaidi duniani.

Utafiti huo umefichua kuwa nyumba 30 za gharama ya juu zaidi duniani huku Saudi Arabia ikiongongoza kwa kuwa na majengo mawili yenye thamani ya juu zaidi yaliyopo Mecca.

Utafiti huo uliofanyika mwaka 2019 ulibaini kuwa msikiti wa Ka'bah uliopo Mecca, na Masjid al-Haram, ndio majengo yenye garama zaidi duniani na makubwa zaidi.

Kupanuliwa kwa msikiti huo kwa miaka kadhaa kumeuongezea thamani zaidi kuliko jengo jingine lolote duniani na kulingana na MSN Money, msikiti huo una thamani ya dola bilioni 100 ($100bn)

Jengo la Abraj Al-Bait lililoko mjini Mecca, ambalo linajumuisha hoteli, makazi ya kifahari na maduka, ndilo la pili lenye garama zaidi duniani likiwa na thamani ya dola bilioni 16 ($ 16 billion)

Majengo ya Maina Bay Sands resorts yaliyopo Singapore niya tatu kwa ukubwa nchini humo yakiwa na thamani ya zaidi ya dola bilioni 6 ( over $ 6 billion)

Jingo la Burj Khalifa, lililopo mjini Dubai katika Milki za kiarabu (UAE) linachukua nafasi ya 30 katika orodha ya majengo ghali zaidi duniani, licha ya kwamba ndio jingo refu kuliko majengo yote duniani.

Majengo 10 yenye gharama zaidi duniani:

Msikiti wa Ka'bah , Makkah: Dola bilioni 100
Eneo hilo takatifu zaidi kwa dini ya Uislamu na msikiti mkubwa zaidi duniani wa Ka'bah mjini Mecca, Saudi Arabia, ambao una uwezo wa kuwapokea watu zaidi ya milioni nne wakati wa Hija ,linakadiriwa kuwa na thamani ya dola bilioni 100.


Abraj Al Bait Building, Makkah: Dola Bilioni
Jengo la Makkah Abraj Al Bait, lililopo karibu na Msikiti wa Ka'aba Mosque, llilojengwa mnamo mwaka 2012,linakadiriwa kuwa na thamani ya dola 16.

Abraj Al Bait lilijengwa kwa garama ya dola bilioni 15 kwa ajili ya kuwahifadhi mahujaji hususan viongozi na matajiri. Zaidi ya hayo ukubwa wake, jingo hilo lina saa kubwa zaidi duniani.

Jengo la Abraj Al Bait ni jengo la pili lenye thamani zaidi duniani baada ya Msikiti wa Ka'bah uliopo Mecca.

Eneo la burudani la Marina Bay Sands, Singapore: dola bilioni 6.2
Eneo la burudani la Marina Bay Sands resort lililopo Singapore lenye hoteli na majumba ya kifahari ndilo linalochukua nafasi ya tatu kati ya majengo yenye gharama ya juu zaidi duniani likiwa na thamani ya dola bilioni 6.2

Marina Bay Sands, ambalo ujenzi wake ulikamilika mnamo mwaka 2010, lilijengwa kwa garama ya ya dola bilioni 5.5 na thaha thamani yake imepanda.

Makao makuu ya kampuni ya Apple, Cupertino: Dola Bilioni 5.
Jengo la Apple Park, makao makuu ya Apple yaliyopo Cupertino, California, ni la nne miongoni mwa majengo ya bei ya juu duniani.

Apple, ambayo ndio kampuni ya gharama zaidi duniani, inasemekana ina mapato ya jumla ya juu zaidi kuliko mali zote zinazomilikiwa na mataifa yanayoendelea.

Si jambo la kushangaza kwamba kampuni ilitumia ilitumia dola bilioni 5 kujenga jingo hilo kubwa la makao yake makuu.

Cosmopolitan Building, Las Vegas: Dola Bilioni 4.4
Ikiwa na jumla ya vyumba 3,027-vya kulala Cosmopolitan Hotel ina thamani ya dola bilioni 3.9 na ujenzi wake ulikamilika mwaka 2009.

Jengo la hotel likiwa na kasino kubwa, chumba cha mikutano chenye viti 3,200- ni jingo la tano lenye gharama zaidi duniani.

New World Trade Center, New York: Dola 4.1 billion
Jengo la New York-World Trade Center linashikilia nafasi ya sita katika orodha ya majengo yenye ghali zaidi duniani kulingana na kampuni ya MSN Money.

Ujenzi wa One World Trade Center ulikamilika mnamo mwaka 2012 kwa garama ya dola bilioni 3.8 (£ 2.7bn), lakini kwa sasa thamani yake imepanda hadi zaidi ya dola bilioni 4.

Jengo hilo kwa sasa ndilo linaloshikilia nafasi ya kwanza kwa ukubwa nchini Marekani.


Jengo la bunge la Bucharest: Dola bilioni 3.9
Jengo hili ambalo lilizinduliwa mwaka 1984, sasa lina thamani ya dola bilioni 3.9. Linapatikana Romania.

Jengo la Hoteli-Emirates Palace Hotel Building, lililoko Abu Dhabi: Dola bilioni 3.8
Jengo hilo la hoteli ambalo muundo wake unafanana na ule wa kasri ya ufalme ya Dubai ina jumla ya vyumba vya kulala 397 pamoja na maduka makubwa (malls) na madogo na migahawa ya kifahari.


Thamani ya jengo hilo ambalo ujenzi wake ulikamilika mwaka 2005, likikadiliwa kuwa na thamani dola billioni 3, kwa sasa thamani yake ni zaidi.

Wynn Resort, Las Vegas: Dola bilioni 3.4
Jengo hili ni mojawapo ya hoteli nzuri zaidi duniani likiwa katika kundi la kasino kubwa katika za Las Vegas.

Mwaka 2005 jengo la Wynn Park lilizinduliwa. Thamani ya jengo hili lenye vyumba 2,716-likikadiliwa kuwa ni dola bilioni 2.7, sasa thamani yake ni zaidi ya dola bilioni 3.4.

Kasri la Mfalme wa Brunei Istana Nurul Iman: Dola Bilioni 3.3
Kasri la Brunei lililojengwa 1984 kwa gharama ya dola bilioni 1.4 billion, ndio kasri kubwa zaidi duniani ambalo bado limesimama kama kasri.

Jengo la kasri la serikali ya Brunei likiwa na vyumba 1,788 na ukumbi mkubwa wa mikutano unaoweza kuwapokea watu 5,000.

Sultan wa Brunei Hassanal Bolkiah ni mmoja wa watu matajiri zaidi duniani.

CHANZO - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments