Picha : MAHAFALI YA 15 YA DARASA LA SABA 2020 SHULE YA MSINGI BUHANGIJA YAFANA

 


Mgeni Rasmi Afisa elimu Taaluma manispaa ya Shinyanga Wingwila Kitila akikata keki kwenye mahali ya 15 ya kuwaaga wanafunzi waliohitimu Darasa la saba mwaka 2020.


Na Marco Maduhu -Shinyanga. 
Shule ya msingi Buhangija iliyopo katika manispaa ya Shinyanga, imefanya mahali ya 15 ya kuwaaga wanafunzi waliohitimu Darasa la saba mwaka 2020.


Mahafali hayo yamefanyika leo shuleni hapo, na kuhudhuriwa na wazazi,walimu, ambapo mgeni rasmi alikuwa Afisa Elimu Taaluma shule za msingi manispaa ya Shinyanga Wingwila Kitila aliyemwakilisha Mkurugenzi wa manispaa hiyo Geofrey Mwangulumbi. 

Akizungumza kwenye mahafali hayo, Kitila amewataka wanafunzi hao pindi watakapoingia kidato cha kwanza, wakaendeleze juhudi za kusoma kwa ajili ya maisha yao ya baadaye, na siyo kwenda kucheza ambapo watajikuta wakizima ndoto zao na kuishia mitaani kuranda randa. 

“Kuhitimu elimu hii msingi ya darasa la saba siyo kwamba ndiyo mmemaliza masomo, bali ndiyo mmeuanza mwendo, mkifika huko Sekondari mkaongeze bidii za kujisomea, pamoja na kuwa na nidhamu ya hali ya juu, ili mpate kufikia ndoto zenu,”alisema Kitila. 

Katika hatua nyingine ameahidi kuitatua changamoto ya upungufu wa walimu maalumu shuleni hapo, ambapo tayari wameshatuma maombi TAMISEMI kuomba walimu, na wanasubili uchaguzi uishe ili ajira zitoke na kuitatua changamoto hiyo. 

Naye afisa elimu Kata ya Ibinzamata Mackline Shija, amewataka wazazi waendeleze malezi bora kwa watoto wao ambao wamehitimu darasa la saba na siyo kuwa acha wakidhurura hovyo mitaani, na kujikuta wakiingia kwenye makundi mabaya na hata kuambulia mimba za utotoni. 

Akisoma risala ya wahitimu , Naziri Vicent, aamesema wamehitimu wanafunzi 110, wavulana wakiwa 54 na wasichana 56, na kubainisha changamoto ambayo wanaicha shuleni hapo ni upungufu wa walimu maalumu.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Mgeni Rasmi Afisa elimu Taaaluma manispaa ya Shinyanga Wingwila Kitila akizungumza kwenye mahali ya 15 ya kuwaaga wanafunzi waliohitimu Darasa la saba mwaka 2020.
Afisa elimu Kata ya Ibinzamata manispaa ya Shinyanga Mackrine Shija, akizungumza kwenye mahali ya 15 ya kuwaaga wanafunzi waliohitimu Darasa la saba mwaka 2020.
Mwalimu mkuu Shule ya Msingi Buhangija Seleman Kipanya, akizungumza kwenye Mahafali hayo na kuipongeza Serikali kwa kujenga uzio kwenye mabweni ya kulea watoto wenye ualbino.
Mhitimu wa Darasa la saba Naziri Vicent akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wenzake.
Wahitimu Darasa la Saba Shule ya Msingi Buhangija wakiwa kwenye Mahafali yao.
Wahitimu Darasa la Saba Shule ya Msingi Buhangija wakiwa kwenye Mahafali yao.
Wahitimu Darasa la Saba Shule ya Msingi Buhangija wakiwa kwenye Mahafali yao.
Wahitimu Darasa la Saba Shule ya Msingi Buhangija wakiwa kwenye Mahafali yao.
Wazazi wakiwa kwenye mahafali ya watoto wao waliohitimu Drasa la Saba.
Wazazi wakiwa kwenye mahafali ya watoto wao waliohitimu Drasa la Saba.
Wazazi wakiwa kwenye mahafali ya watoto wao waliohitimu Drasa la Saba.
Wazazi wakiwa kwenye mahafali ya watoto wao waliohitimu Drasa la Saba.
Walimu Shule ya Msingi Buhangija wakiwa kwenye mahafali.
Walimu Shule ya Msingi Buhangija wakiwa kwenye mahafali.
Keki maalumu kwa ajili ya wahitimu Darasa la Saba Shule ya Msingi Buhangija.
Mgeni Rasmi Afisa elimu Taaluma manispaa ya Shinyanga Wingwila Kitila akikata keki kwenye mahali ya 15 ya kuwaaga wanafunzi waliohitimu Darasa la saba mwaka 2020.
Mgeni Rasmi akitoa vyeti kwa wahitimu Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Buhangija.
Zoezi la utoaji vyeti likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti likiendelea.
Mgeni Rasmi, akitoa cheti cha pongezi kwa Muhitimu Naziri Vicent, aliyefanya vizuri kitaaluma Shuleni hapo kwa upande wa wavulana.
Mgeni Rasmi akitoa cheti cha pongezi kwa Mwanafunzi Amina Mhina, aliyefanya vizuri kitaaluma shuleni hapo kwa upande wa wasichana.
Wahitimu Darasa la Saba wakitoa burudani kwenye mahafali hayo.
Burudani ikiendelea kutolewa.
Wanafunzi wanaobaki shule wakitoa burudani ya mitindo.
Wanafunzi wanaobaki shule wakitoa burudani kwenye mahafali hayo.
Burudani ikiendelea kutolewa.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments