TUNDU LISSU ATAKIWA KUFIKA MBELE YA KAMATI YA MAADILI YA NEC

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemuandikia barua mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu ya kumuita katika kikao cha kamati ya maadili ya Taifa.


Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dkt. Charles Mahera amesema hilo leo jijini Arusha wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo ameeleza kuwa mgombea huyo atafika mbele ya kamati Septemba 29 mwaka huu.

Akizungumzia uratibu na usimamizi wa kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu amesema tume imekumbana na changamoto kwa baadhi ya wagombea wa kiti cha Rais kutoheshimu sheria, taratibu na maadili ya uchaguzi.

Ameongeza kuwa baadhi ya wagombea wamekuwa wakitumia maneno ya kukashifu wagombea wenzao, tume, pamoja na kutoa taarifa zisizo za kweli zenye lengo la kuleta taharuki na uzushi miongoni mwa Watanzania.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527