SUMAYE AISHUKIA CHADEMA, ASEMA HAWAWEZI KUONGOZA NCHI


Na John Walter-Hydom, Mbulu
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Frederick Sumaye amesema vyama vya Upinzani nchini haviwezi kuongoza nchi kwa sababu hawana sera.

Ameyasema hayo Leo Septemba 30,2020 akizungumza na wananchi wa Jimbo la Mbulu Vijijini katika mkutano wa Mgombea Mwenza Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia  Suluhu Hassan kunadi Sera za  Chama cha Mapinduzi katika viwanja Vya Haydom.

Sumaye amesema Chama alichotoka  CHADEMA,  ni Chama cha Uwana harakati na hakina sera  zozote za kuwasaidia wananchi.

'CHADEMA wanafikiri kuwa nchi ya Tanzania bado ipo  mikononi mwa  Wakoloni, wanapiga kelele utafikiri bado tunatawaliwa' alisema Sumaye

'Nilienda kule  lakini baada ya kugundua hawana chochote nikaamua kurejea nyumbani' alisisitiza Sumaye

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Manyara Simon Lulu amesema Chama hicho kinajiandaa kwa ushindi wa kishindo kwa sababu kimefanya maendeleo kwa wananchi.

Amemweleza Mgombea Mwenza kiti  cha Urais Tanzania Samia Suluhu Hassan kwamba katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba 28 mwaka huu, Upinzani mkoani hapo hawataambulia hata kiti  cha Udiwani.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments