NHIF ZANZIBAR YAHAMASISHA UMUHIMU WA BIMA YA AFYA NA MAZOEZI | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, September 12, 2020

NHIF ZANZIBAR YAHAMASISHA UMUHIMU WA BIMA YA AFYA NA MAZOEZI

  TANGA RAHA BLOG       Saturday, September 12, 2020
MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Zanzibar Ismail Nuhu Kangeta akizungumza wakati wa Bonanza la michezo kwa watumishi wa Serikali na wananchi Zanzibar lililofanyika kwenye viwanja vya Mau mjini Unguja

MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Zanzibar Ismail Nuhu Kangeta katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa bonanza hilo
Washiriki wa Bonanza hilo wakiendelea na mazoezi kwenye viwanja hivyo
Sehemu ya wananchi waliojitokeza kwenye bonana hilo

NA MWANDISHI WETU,ZANZIBAR.

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya Zanzibar umehamasisha wananchi kujiunga na mfuko huo ili kuweza kunufaika na huduma mbalimbali zinazotolewa sambamba na ufanyaji wa mazoezi kila wakati kwa ajili ya kupambana na magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo kisukari na shinikizo la damu.

Hayo yalisemwa na Meneja Mkaazi wa ofisi ya ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Zanzibar Ismail Kangeta wakati akitoa elimu ya umuhimu wa bima ya afya wakati wa bonanza ambalo liliandaliwa na Mfuko huo ofisi ya Zanzibar.

Bonanza hilo lilikwa na lengo la kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya Afya pia kusisitiza umuhimu wa kushiriki kwenye michezo ili kupunguza magonjwa yasiyoambukizwa ambayo ndio yamekuwa tishio kwa afya za watu kwa sasa.

"Kama unavyojua ukifanya mazoezi mara kwa mara kuna uwezekano mkubwa wa kuepukana na magonjwa yasiyoyakuambukiza hivyo ndio maana tumeona tuandae bonanza hili na litakuwa linafanyika kila wakati"Alisema.

Hata hivyo aliwataka wananchi kujiunga na mfuko huo ili kuweza kunifaika na huduma mbalimbali ambazo wamekuwa wakizitoa

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post