BOTSWANA KUANZA KUTUMIA LUGHA YA KISWAHILI SHULENI


Serikali ya Botswana inakusudia kuanzisha matumizi ya lugha ya Kiswahili katika Shule za Msingi. Waziri wa Elimu ya Msingi, Fidelis Molao amesema matumizi ya lugha ya Kiswahili yataanzishwa katika Shule ndani ya siku chache  zijazo.

Kiswahili ni lugha ya Kibantu inayozungumzwa sana katika eneo la Maziwa Makuu na sehemu zingine za Mashariki na Kusini Mashariki mwa Afrika ikiwa ni pamoja na Kenya, Tanzania, Burundi, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na sehemu za Malawi.

Ikiwa Kiswahili kitatumika Botswana itakuwa ni lugha ya kwanza ya Kiafrika kutumika kutoka nje ya mipaka ya nchi hiyo ambayo ni mzalishaji mkubwa wa Almasi Ulimwenguni.

Molao amesema, Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) itakuwa na washirika wakubwa wa kibiashara na nchi nyingi zinazozungumza Kiswahili katika siku za usoni jambo ambalo hata Botswana inalihitaji zaidi katika kukuza uchumi na mauzo ya nje.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527