ATIWA MBARONI AKITUHUMIWA KUCHOMA MOTO BASI LAKE


Jeshi la polisi mkoani Morogoro linamshikilia mmiliki wa mabasi ya ya kampuni ya HBS AHMAD ALLY HEMED na dereva wa kampuni hiyo kwa tuhuma za kuchoma moto kwa makusudi basi lake lenye namba za usajili T.321 DKW aina ya Golden Dragon kisha kudanganya jeshi la polisi kuwa basi hilo limewaka moto baada ya kupata hitilafu kwenye breki wakati likitokea Dar es salaam kuelekea mkoani Dodoma katika eneo la Wami Luhindo wilayani Mvomero.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Wilbroad Mutafungwa amesema tukio hili lilitokea Agosti 27 mwaka huu na kwamba baada ya kupata taarifa za kuwepo kwa tukio hilo walishirikiana na Jeshi la zimamoto na uokoaji kuzima moto huo na baadae kufanya uchunguzi wa kina na kubaini kuwa basi hilo halikuwa na injini,chasesi wala viti vya abiria.

Aidha Kamanda Mutafungwa ameeleza kuwa baada ya mahojiano ya muda mrefu watuhumiwa hao wamekiri kudanganya Jeshi la Polisi na kutoa sababu kuwa mmiliki anadaiwa zaidi ya shilingi milioni 200 na alifanya hivyo ili aweze kulipwa na moja ya kampuni ya bima pesa ambazo zingeweza kumsaidia kulipa deni hilo na kwamba alilazimika kulisafirisha basi hilo likiwa bovu kutoka jijini Dar es Salaam kwa lori namba T 336 DDX


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527