MWANAFUNZI AMKATA PANGA MWALIMU WAKE | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, September 24, 2020

MWANAFUNZI AMKATA PANGA MWALIMU WAKE

  Malunde       Thursday, September 24, 2020

Jeshi la polisi mkoani Mara linamshikilia mwanafunzi wa kidato cha tatu Mwita Machamo,(17) katika shule ya sekondari ya Kiagata kwa kumkata na panga mwalimu wake Majogoro John, baada ya mwanafunzi huyo kushindwa kumpeleka mzazi wake shuleni kama alivyoagizwa na mwalimu.


Taarifa hiyo imetolewa leo Septemba 24, 2020, na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara Daniel Shillah, na kusema kuwa tukio hilo lilitokea shuleni hapo majira ya asubuhi wakati mwalimu anakagua wanafunzi watoro, na ndipo mwanafunzi huyo alimgeukia mwalimu wake na kumkata mapanga.

"Baadhi ya wanafunzi waliwaleta wazazi wao, lakini huyu mwanafunzi kwa utovu wa nidhamu uliopindukia alikuja na upanga akiwa ameuficha kwenye nguo zake na mwalimu alipohoji kwanini hujaja na mzazi, mwanafunzi akachomoa upanga na kumshambulia mwalimu na akawatisha tisha wanafunzi wengine akapata nafasi ya kukimbia lakini wakamkata na tumemshikilia na atafikishwa mahakamani", amesema Kamanda Shillah.

Majogoro John ni mwalimu aliyejeruhiwa na mwanafunzi wake hapa amesimulia hali ilivyokuwa:

"Nilipita darasani kuangalia watoro nikamambia fuata mzazi tuje tuongee ili nijue shida nini yule akatembea hatua kama tatu kwenda mlangoni akageuka alivyotoa upanga akageuka haraka akanikata begani akageuka tena ili anikate kichwani ndipo nikaweka mkono wa kushoto akaiga panga nikaona tu mkono unaning'inia".

Kwa upande wake mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara Joachim Iyembe, amesema kuwa wamempokea mgonjwa huyo na kumpa rufaa ya kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi.

 Chanzo - Eatv
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post