Picha : EMMANUEL NTOBI AZINDUA RASMI KAMPENI ZA CHADEMA NGOKOLO...AMUOMBEA KURA LISSU, MAKAMBA





Mgombea udiwani Kata ya Ngokolo Chadema, Emmanuel Ntobi, (kulia) akijiombea kura na kumuombea kura kwa wananchi wa Ngokolo Salome Makamba, kuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini 


Na Marco Maduhu -Shinyanga.
Mgombea udiwani wa Kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Emmanuel Ntobi amezindua rasmi Kampeni zake za uchaguzi mkuu 2020 huku akitoa ahadi ya kuboresha sekta ya elimu, afya, kujenga Soko, kituo cha Polisi, barabara, pamoja na kuanzisha Saccos ya kata ili kuinua wananchi kiuchumi.


Ntobi amezindua rasmi kampeni zake kwenye Kata ya Ngokolo, mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Ngokolo mitumbani ambapo uzinduzi huo umehudhuriwa pia na Mgombea ubunge wa Jimbo la Shinyanga mjini kupitia (CHADEMA) Salome Makamba.

Amesema ndani ya miaka mitano katika uongozi wake akiwa diwani wa Kata hiyo ya Ngokolo, kuna vitu vingi ambavyo amevifanya kwa ajili ya maendeleo ya wananchi, na kuomba wampe tena mitano mingine ili kamilishe miradi mingine ambayo alikuwa ameianza pamoja na kuinua wananchi kuichumi kwa kuanzisha Saccos ya Kata.

“Kwenye uongozi wangu nilipokuwa diwani kuna vitu vingi ambavyo nimevifanya ukiwemo ujenzi wa Ghuba, kukarabati shule mbili za msingi Mwadui na Mapinduzi, kujenga kituo cha Polisi mtaa wa Majengo ambacho kipo kwenye hatua za mwisho, ujenzi wa barabara kiwango cha Lami, na utatuzi wa migogoro,” amesema Ntobi.

“Pia nilitafuta wafadhili kutoka Denmark walinipatia vifaa tiba, vikagawiwa kwenye maeneo mbalimbali ya huduma za afya hapa manispaa ya Shinyanga, ambapo tena vifaa hivyo vilitumwa lakini mpaka sasa vimezuiliwa bandarini,” ameongeza.

Aidha alitaja vipaumbele vyake endapo wananchi watamchagua tena kuwa diwani wao kuwa atajenga kituo cha afya, kumalizia kituo cha Polisi, kuboresha sekta ya elimu , kujenga Soko, Garden ya kupumzikia wananchi , pamoja na kuanzisha Saccos ya Kata ambayo itasaidia kuinua uchumi wa wananchi.

Katika hatua nyingine alitaja sababu za kufukuzwa mara kwa mara kwenye vikao vya baraza la madiwani la manispaa ya Shinyanga, kuwa inatokana na kupigania masuala ya ufisadi ikiwamo kupinga ungezeko la Tozo kwenye vibanda vinavyomilikiwa na manispaa ya Shinyanga, na kubainisha kuwa jambo hilo pia hata Rais John Magufuli alilisema alipokuwa Shinyanga akizindua kampeni za uchaguzi.

Alisema kitu kingine ni kupinga kupandishwa wananchi bei ya kuuziwa viwanja na manispaa ya Shinyanga, kutoka Shilingi Laki Tano hadi Milioni 2, na kudai aliundiwa njama za kutolewa nje ya kikao ili bajeti hiyo ipitishwe.

Kwa upande wake mgombea ubunge wa jimbo la Shinyanga mjini Salome Makamba kupitia chama hicho, amewataka wananchi wa Kata hiyo wasifanye makosa siku ya Jumatano Oktoba 28, bali wampigie kura Emmanuel Ntobi ili awe diwani pamoja na yeye kuwa mbunge , na Mgombea urais Tundu Lissu ili wakafanye kazi pamoja ya kuwaletea maendeleo.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI


Mgombea udiwani Kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi akinadi Sera kwa wananchi leo Jumanne Septemba 15,2020 wakati akizindua rasmi kampeni za uchaguzi.

Mgombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Salome Makamba akizungumza na wananchi wa Kata ya Ngokolo.

Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Shinyanga Khamisi Ngunila, akiomba kura kwa wananchi wa Shinyanga kuwapigia kura wagombea wote wa udiwani kutoka Chadema, Mbunge Salome Makamba pamoja na Rais Tundu Lissu.

Awali viongozi wa Chadema, na wafuasi wa chama hicho, wakiwa na mgombea udiwani Kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi.

Wananchi wa Kata ya Ngokolo wakiwa kwenye Kampeni za mgombea udiwani wa Kata hiyo Emmanuel Ntobi wakisikiliza Sera zake.

Wananchi wa Kata ya Ngokolo wakiwa kwenye Kampeni za mgombea udiwani wa Kata hiyo Emmanuel Ntobi wakisikiliza Sera zake.

Wananchi wa Kata ya Ngokolo wakiwa kwenye Kampeni za mgombea udiwani wa Kata hiyo Emmanuel Ntobi wakisikiliza Sera zake.

Wananchi wa Kata ya Ngokolo wakiwa kwenye Kampeni za mgombea udiwani wa Kata hiyo Emmanuel Ntobi wakisikiliza Sera zake.

Wananchi wa Kata ya Ngokolo wakiwa kwenye Kampeni za mgombea udiwani wa Kata hiyo Emmanuel Ntobi wakisikiliza Sera zake.

Mgombea udiwani Kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi, mwenye gwanda, akiwa na Mgombea ubunge Jimbo la Shinyanga mjini Salome Makamba, mara baada ya kumaliza kuzindua Kampeni kwenye Kata hiyo.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527