" VICTOR MKWIZU AZINDUA RASMI KAMPENI ZA UCHAGUZI CCM NGOKOLO...KATAMBI, ABUBAKARI WAOMBA KURA

VICTOR MKWIZU AZINDUA RASMI KAMPENI ZA UCHAGUZI CCM NGOKOLO...KATAMBI, ABUBAKARI WAOMBA KURAMgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CCM Patrobas Katambi akijiombea kura na kumuombea Victor Mkwizu (kulia) kuwa diwani wa kata ya Ngokolo na Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Tanzania ili kuleta maendeleo katika kata ya Ngokolo. Kushoto ni 
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga mjini Abubakari Gulam


Na Suzy Luhende - Shinyanga
Mgombea Udiwani kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM  Victor Mkwizu amewaomba wananchi wa kata ya Ngokolo kumchagua ili aweze kuondoa kero zilizopo katika kata hiyo na kuleta maendeleo kwa kushirikiana na Mbunge Patrobas Katambi wakishirikiana na Rais John Pombe Magufuli.

Akizindua kampeni zake za kuwania udiwani kata ya Ngokolo iliyofanyika  leo Alhamis Septemba 17,2020 katika viwanja vya mtaa wa Mageuzi kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga, Mkwizu aliwaomba wananchi wote wa kata hiyo kumchagua yeye awe diwani, kumchagua Patrobas Katambi awe mbunge na kumchagua Rais John Pombe Magufuli ili waweze kushirikiana na kuziondoa kero zilizopo na kuleta maendeleo.

Victor alisema atakapochaguliwa kipaumbele chake atahakikisha anasimamia zahanati inajengwa, kina mama watapatiwa mikopo kwa wakati na soko la Ngokolo  litajengwa kwa sababu eneo limeshatengwa ili akina mama waweze kufanya biashara na kujikwamua kiuchumi.

Pia kipaumbele kingine amesema atahakikisha kituo cha polisi kina jengwa katika kata hiyo  kwa ajili ya usalama zaidi na kutengenezea barabara zote ambazo hazipitiki wakati wa mvua kwa kushirikiana na mbunge Katambi na Rais John Pombe Magufuli.

"Ndugu zangu wananchi wa kata ya Ngokolo nawaombeni sana mnichague Mimi niwe diwani wenu, mmchague mbunge Katambi na Rais Magufuli ili tuweze kuwatumikia na kuhakikisha tunaondoa kero zote zilizopo Katika kata  yetu,kwa kushirikiana kwa pamoja tutaleta maendeleo na kuifanya Ngokolo yetu inakuwa mpya,"alisema Mkwizu.

"Hatutaishia hapo pia tutashughulikia mikopo ya akina mama vijana na walemavu iweze kuwafikia akina mama walemavu, na vijana ili kuondoa umasikini kwa watu wote wa kata ya Ngokolo na tutafanya vikao mara kwa mara vya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi ili kuweza kuzitatua kwa wakati",alisisitiza Mkwizu.

Kwa upande wake Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi aliyehudhuria pia uzinduzi huo aliwaomba wananchi wote wa kata ya Ngokolo na Jimbo kwa ujumla wamchague ili aweze kuwaletea maendeleo kwa sababu ni mchapa kazi anajitambua.

"Wazazi wangu wapendwa na ndugu zangu nimekuja tena kwa mara  nyingine kwa heshima na taadhima, nawaombeni kura zenu zote mmpe Victor mgombea udiwani kupitia CCM na mnipe mimi niwe mbunge wenu kupitia CCM na mmpe Rais wetu mpendwa anayeshangaza Africa nzima kwa kufanya maendeleo na kuifikisha nchi ya Taifa katika uchumi wa kati",alisema Katambi.

Katambi alisema akichaguliwa atahakikisha anaongeza madarasa ya shule za msingi na sekondari ili wasiendelee kubanana kwa ajili ya afya zao na waweze kufaulu vizuri kwa sababu ndio viongozi wa kesho.

"Watoto wetu wanasoma huku wakiwa wamebanana sana madarasani, hivyo mkinichagua lazima kipaumbele changu tuongeze madarasa,vyoo na shule za kulala wanafunzi  ili waweze kusoma kwa kujiamini na ufaulu uongezeke, naombeni tu tarehe 28 Oktoba msikosee nichagueni ili niwaletee maendeleo ya Ngokolo",alisema Katambi.

Pia alisema akichaguliwa hatawasahau kina mama, atasimamia mikopo yao kwa karibu ili kuhakikisha asilimia nne wanapatiwa kina mama na asilimia nne ya vijana wanapatiwa pamoja na asilimia mbili ya walemavu. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Abubakari Gulam aliwaomba wananchi wa Ngokolo wachague mafiga matatu ambao ni diwani Mkwizu CCM, mbunge Katambi CCM na Rais John Pombe Magufuli CCM kwa ajili ya kuleta mabadiliko Ngokolo na Jimbo la Shinyanga na Tanzania kwa ujumla.

Baadhi ya wananchi wa kata ya Ngokolo Letisia Jishosha na Ditrick Richard  walisema wanamjua vizuri Victor aliwahi kuwa mwenyekiti wa vijana wilaya ya Shinyanga alikuwa mchapa kazi mzuri hivyo wanaimani nae atashinda kwa kishindo na Katambi ni mleta maendeleo wakishirikiana na Rais Magufuli mabadiliko yatatokea.

Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CCM Patrobas Katambi akijiombea kura na kumuombea Victor Mkwizu (kulia) kuwa diwani wa kata ya Ngokolo na Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Tanzania ili kuleta maendeleo katika kata ya Ngokolo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga mjini Abubakari Gulam. Picha zote na Suzy Luhende - Shinyanga
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CCM Patrobas Katambi akijiombea kura na kumuombea Victor Mkwizu (kulia) kuwa diwani wa kata ya Ngokolo na Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Tanzania ili kuleta maendeleo katika kata ya Ngokolo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga mjini Abubakari Gulam
Mgombea Udiwani kata ya Ngokolo Victor Mkwizu (kulia) akinadi sera zake na kuomba wananchi wamchague kuwa diwani wa kata ya Ngokolo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga mjini Abubakari Gulam
Mgombea Udiwani kata ya Ngokolo Victor Mkwizu (kulia) akinadi sera zake na kuomba wananchi wamchague kuwa diwani wa kata ya Ngokolo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga mjini Abubakari Gulam

Mgombea Udiwani kata ya Ngokolo Victor Mkwizu (kulia) akinadi sera zake na kuomba wananchi wamchague kuwa diwani wa kata ya Ngokolo. Kushoto ni 
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga mjini Abubakari Gulam
Mgombea Udiwani kata ya Ngokolo Victor Mkwizu (kulia) akinadi sera zake na kuomba wananchi wamchague kuwa diwani wa kata ya Ngokolo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga mjini Abubakari Gulam

Mwenyekiti wa chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga mjini Abubakari Gulam akimuombea kura mgombea udiwani kata ya Ngokolo kupitia CCM Victor Mkwizu, na Patrobas Katambi mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na Mgombea Urais Dkt. John Pombe Magufuli.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga mjini Abubakari Gulam akimuombea kura mgombea udiwani kata ya Ngokolo kupitia CCM Victor Mkwizu, na Patrobas Katambi mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na Mgombea Urais Dkt. John Pombe Magufuli.

Wananchi wa kata ya Ngoko wakiwa kwenye uzinduzi wa udiwani wakiserebuka kwenye mkutano wa Kampeni
Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527