Angalia Picha : PATROBAS KATAMBI AZINDUA KWA KISHINDO KAMPENI ZA UCHAGUZI CCM SHINYANGA MJINI

Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi akizungumza wakati wa kuzindua kampeni zake leo katika viwanja vya Ngokolo Mjini Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi amezindua rasmi Kampeni za Uchaguzi Mkuu leo Jumapili Septemba 13,2020 katika viwanja vya Ngokolo kata ya Ngokolo.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na maelfu ya wakazi wa Shinyanga wakiwemo waliokuwa watia nia kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini wakiongozwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Gaspar Kileo ‘Gaki’ ambaye ni Meneja Kampeni wa Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi.

Akinadi sera za Chama Cha Mapinduzi, Katambi amesema endapo atachaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini atahakikisha anaboresha sekta ya kilimo na ufugaji,afya,michezo,elimu,biashara na uwekezaji ili kuwaletea maendeleo wananchi.

Katambi ametumia fursa hiyo kumuombea kura mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na madiwani wote wa CCM akisisitiza kuwa yeye ni mtu wa kazi asiyependa masihara hivyo wananchi wampe kura ili awatumikie kwa kuwaletea maendeleo.

Ameitaja baadhi ya mikakati ya kuinua uchumi wa wananchi kuwa ni kuliendeleza ombi alilolitoa kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la kujengwa kwa Chuo Kikuu katika manispaa ya Shinyang hali ambayo itasaidia kuwepo kwa mzunguko mkubwa wa fedha na kuongeza ajira kwa wananchi. 

Meneja Kampeni wa Patrobas Katambi, Gaspar Kileo amesema Chama Cha Mapinduzi kitafanya Kampeni za Kistaarabu huku akiwaonya wanaochana na wanaopanga kuchana mabango ya mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuacha mara moja.

Aidha Kileo ameeleza kuwa watia nia 59 kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga akiwemo aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Stephen Masele wanamuunga mkono Katambi na kwamba Katambi ndiye anatosha kuwa mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini.

Naye Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa licha ya kueleza kukerwa na taarifa za mabango ya wagombea wa CCM kuchanwa pia amewasihi wanaCCM kuchagua wagombea wa CCM kuanzia ngazi ya Rais, Ubunge na udiwani ili kupata mafiga matatu ambayo yatashirikiana kuleta maendeleo kwa wananchi.

Kwa upande wake, mgombea Udiwani kata ya Ngokolo kupitia CCM Victor Yessaya Mkwizu amewaomba wananchi wa kata ya Ngokolo wamchague kuwa diwani ili ashirikiane nao kusogeza huduma za afya,kutatua kero za wananchi,kuboresha miundombinu ya barabara,elimu,maji,makazi,umeme na michezo sambamba na kuelimisha na kurasimisha vikundi vya wajasiriamali akina mama,vijana na walemavu ili wapate mikopo isiyo na riba kuinua kipato.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI

Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM, Patrobas Katambi (katikati) akiwasili katika viwanja vya Ngokolo kata ya Ngokolo akiwa ameambatana na viongozi na wanachama wa CCM kwa ajili ya kuzindua rasmi Kampeni za Uchaguzi Mkuu Jimbo la Shinyanga Mjini leo Jumapili Septemba 13,2020 . Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM, Patrobas Katambi akinadi sera za CCM na kuomba achaguliwe kuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini leo Jumapili Septemba 13,2020 kwenye viwanja vya Ngokolo wakati wa uzinduzi rasmi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu Jimbo la Shinyanga Mjini.

Wananchi wakimsikiliza Patrobas Katambi
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM, Patrobas Katambi akinadi sera za CCM na kuomba achaguliwe kuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini leo Jumapili Septemba 13,2020 kwenye viwanja vya Ngokolo wakati wa uzinduzi rasmi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu Jimbo la Shinyanga Mjini.

Wananchi wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi CCM
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za CCM Jimbo la Shinyanga Mjini
Wananchi wakimsikiliza Patrobas Katambi wakati akiomba kura achaguliwe kuwa mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini.
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM, Patrobas Katambi akinadi sera za CCM na kuomba achaguliwe kuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini leo Jumapili Septemba 13,2020 kwenye viwanja vya Ngokolo wakati wa uzinduzi rasmi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu Jimbo la Shinyanga Mjini.
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM, Patrobas Katambi akinadi sera za CCM na kuomba achaguliwe kuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini leo Jumapili Septemba 13,2020 kwenye viwanja vya Ngokolo wakati wa uzinduzi rasmi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu Jimbo la Shinyanga Mjini.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa (kulia) akimuombea kura Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM, Patrobas Katambi 
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa  akizungumza kwenye mkutano wa uzinduzi rasmi Kampeni za Uchaguzi Mkuu Jimbo la Shinyanga Mjini leo Jumapili Septemba 13,2020.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa (kulia) akimuombea kura Mgombea Udiwani kata ya Ngokolo Victor Mkwizu

Mgombea Udiwani kata ya Ngokolo Victor Mkwizu akiwaomba wananchi wa kata ya Ngokolo wamchague kuwa diwani wa kata hiyo.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa  akiwatambulisha wagombea ubunge Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga na Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi (kulia) kwenye mkutano wa uzinduzi rasmi Kampeni za Uchaguzi Mkuu Jimbo la Shinyanga Mjini leo Jumapili Septemba 13,2020.
Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga akizungumza kwenye mkutano wa uzinduzi rasmi Kampeni za Uchaguzi Mkuu Jimbo la Shinyanga Mjini leo Jumapili Septemba 13,2020 . 
Wananchi na Wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi rasmi Kampeni za Uchaguzi Mkuu CCM Jimbo la Shinyanga Mjini
Mgombea ubunge viti Maalumu Christina Mzava akimuombea kura kwa kupiga magoti Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi (kulia)
Mgombea ubunge viti Maalumu Santiel Kirumba akimuombea kura Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi (kulia)
Wananchi na Wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi rasmi Kampeni za Uchaguzi Mkuu CCM Jimbo la Shinyanga Mjini
Meneja Kampeni wa Patrobas Katambi, Gaspar Kileo akizungumza kwenye mkutano wa uzinduzi rasmi Kampeni za Uchaguzi Mkuu Jimbo la Shinyanga Mjini leo Jumapili Septemba 13,2020. Gaspar Kileo amesema Chama Cha Mapinduzi kitafanya Kampeni za Kistaarabu 

Meneja Kampeni wa Patrobas Katambi, Gaspar Kileo akiwa na Makada wa CCM waliokuwa wametia nia kugombea ubunge Shinyanga Mjini ambao kwa pamoja wamekubaliana kumuunga mkono Patrobas Katambi. 
Salum Mirambo aliyekuwa mtia nia kugombea ubunge Shinyanga akielezea namna walivyojipanga kuhakikisha Katambi anashinda kwenye uchaguzi mkuu na kuwa mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini.
Aliyekuwa Kada wa CHADEMA Lydia Lefi akirudisha bendera na kadi ya CHADEMA na kujiunga CCM 

Viongozi mbalimbali wa CCM wakiwa kwenye uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi CCM, Kulia ni Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Stephen Masele

Uzinduzi wa kampeni za CCM ukiendelea
Uzinduzi kampeni za Uchaguzi CCM ukiendelea
Meza kuu wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea wakati wa uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi CCM 
Wagombea udiwani kata mbalimbali katika jimbo la Shinyanga Mjini wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi rasmi Kampeni za Uchaguzi Mkuu Jimbo la Shinyanga Mjini leo Jumapili Septemba 13,2020 . 

Viongozi mbalimbali wa CCM wakiwa jukwaa kuu
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Abubakar Gulam akizungumza kwenye mkutano wa uzinduzi rasmi Kampeni za Uchaguzi Mkuu Jimbo la Shinyanga Mjini leo Jumapili Septemba 13,2020 . 
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM mkoa wa Shinyanga Richard Msanii akizungumza kwenye mkutano wa uzinduzi rasmi Kampeni za Uchaguzi Mkuu Jimbo la Shinyanga Mjini leo Jumapili Septemba 13,2020 . 
Wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi rasmi Kampeni za Uchaguzi Mkuu Jimbo la Shinyanga Mjini leo Jumapili Septemba 13,2020.

Waandishi wa habari na wananchi wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi rasmi Kampeni za Uchaguzi Mkuu CCM Jimbo la Shinyanga Mjini.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blogDownload/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post