PROFESA KITILA AVUTIA WENGI, AAHIDI MAGEUZI MAKUBWA JIMBO LA UBUNGO



Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ubungo kupitia CCM, ) Profesa Kitila Mkumbo

Na Godwin Myovela, Dar es Salaam.
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Ubungo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Profesa Kitila Mkumbo amewahakikishia wana-ubungo wa vyama vyote kuwa endapo watamparidhaa ya uwakilishi atashughulikia kero za maji, miundombinu ya barabara za mitaa, uboreshaji wa mifumo ya uendeshaji wa masoko, sambambana kurasimisha shughuli za waendesha bodaboda na bajaji kuwa kazi rasmi tofauti na ilivyo sasa.


Aidha, amesema kadri atakavyojaliwa na Mwenyezi Mungu atahakikisha anachagiza ustawi wa Kiwanda cha nguo cha Urafiki ambacho kwa sasa kinaendeshwa kwa kusuasua ili kiwe mhimili wa ajira kwa vijana na ustawi wa maendeleo kwa tija ya wana-ubungo wote na taifa kwa ujumla. 

Profesa Mkumbo aliyasema hayo jana wakati akinadi sera, ilani ya CCM na shabaha ya shughuli zake za kibunge kwa wakazi wa Shirika la Nyumba na maeneo ya Urafiki, Kata yaUbungo, kwenye viwanja vya Kinesi jijini Dar es Salaam.

“Kiwanda chetu cha Urafiki mpaka sasa kinaendeshwa kwa kusuasua na wasihi ni kiwaomba mnipe ridhaa ili niwesehemu kubwa ya ushawishi wa kuleta ustawi mpya wa kiwanda cha  Urafiki ambacho kwa sasa kinaendeshwa kwa kusuasua ili kiwe mhimili wa ajira kwa vijana na ustawi wa maendeleo kwa tija  kwa wana ubungo wote na taifa kwa ujumla ,” alisema Mkumbo.

Akifafanua dhana ya kurasimisha ajira za vijana takribani elfu 3 waliojiajiri kuendesha bodaboda na bajaji waliopo ndani ya jimbo la ubungo, Profesa Mkumbo alisema atahakikisha kazi hiyo inarasimishwa na kuwa ajira rasmi itakayoanza  kuheshimika na mamlaka zote zilizopo ili kulinda haki na maslahi stahiki ya vijana hao kwa uwiano na tija tarajiwa.

“Haiwezekani nasio sawa hata kidogo bodaboda na bajaji akikamatwa na askari apewi ‘notifications’ yoyote anawekwandani na chombo chake pia kinazuiliwa…siosawa,” alisema Profesa Mkumbo huku akishangiliwa na mamia ya waendesha bodaboda na bajaji waliohudhuria mkutano huo. 

“Mbona madereva wa magari wanapewa mda wa hadi siku saba kulipa faini?” alihoji.

Akizungumzia kero za ubovu wa miundombinu ya barabara za mitaa alisema endapo wana-ubungo watampa ridhaa atahakikisha anashawishi kufanyika maboresho na matengenezo ya uhakika ya barabara zote korofi ndani ya jimbo hilo kwa kujenga hoja kwenye Baraza la Halmashauri kuanza kutenga walau asilimia 3 mpaka 5 ya mapato yake ili kushughulikia kero hiyo.

Profesa alisema mpaka sasa sehemu ya takribani kilo meta 35 za mtandao wa barabara za jimbo hilo ambazo hazipitiki zimeingizwa kwenye mpango maalumwa maboresho, huku akisisitiza endapo atachaguliwa atakoleza kasi hiyo ya utatuzi wa kero za barabara za mitaa kwa kutumia fedha za Mfuko wa Jimbo ambazo kila mwananchi wa ubungo atakuwa na haki ya kuhoji zimetumikaje.

Kuhusu uboreshaji wa masoko alisema endapo atapewa ridhaa atahakikisha anashawishi viongozi na wadau ilikubadilisha mfumo wa uendeshaji na kufanya maboresho kwenye masoko ya Big Brother, Simu2000 na soko kubwa maarufu la Ndizi lililopo eneo la Mabibo na idara zake ili kuwa na tija zaidi na kuleta mageuzi kwa kunufaisha walengwa.

Hata hivyo, mgombea huyo ubunge wa Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya CCM hakuliacha nyuma suala la michezo ambapo mkakati wake mkubwa nikuhakikisha anakomboa uwanja wa TP uliopo Sinza ili utumike na wana jimbo hilo kwa shughuli za michezo, sambamba na kukarabati uwanja wa Kinesi ili uweze kutumika rasmi kwa shughuli mbalimbali zakijimbo.

“Nafahamu vijana wengi wanahitaji mlezi ambaye ni mbunge kwenye michezo, endapo mtanichagua nitakuwa mlezi wa vijana kwenye michezo na ninahakika tutafika sehemu nzuri…pia tuna mpango wa kuboresha mikopo kwa kinamama na wajasiriamali…chagueni CCM, chagueni Mbunge wa CCM ilikuvutia serikali kuleta maendeleo kwenye jimbo hili,” alisema Profesa Mkumbo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527