Picha : AGAPE YATOA ELIMU YA LISHE BORA KWA WATOTO KWA AKINA MAMA DIDIA



Shirika lisilo la kiserikali la AGAPE ACP ambalo linatetea haki za wanawake na watoto mkoani Shinyanga, kwa kushirikiana na Serikali limetoa elimu kwa akina mama wa Kata ya Didia halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, namna ya kuzingatia Lishe bora kwa watoto wao, ili kukabiliana na magonjwa mbalimbali ikiwamo udumavu, pamoja kinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.


Elimu hiyo imetolewa leo Ijumaa Septemba 11,2020 katika eneo la Didia na kukutanisha wanawake 40 kutoka kwenye vijijini vitano vya kata hiyo, kila kijiji kikiwa na akina mama wanne wenye watoto walio na umri chini ya miaka sita, ili wakawe mabalozi kwa wenzao, ambapo pia wamefundishwa namna ya kulima viazi Lishe pamoja na matumizi yake.

Akizungumza kwenye mafunzo hayo mkurugenzi Mtendaji wa Shirika  la AGAPE ACP John Myola, amesema wametoa mafunzo hayo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wao wa uboreshaji wa Lishe bora kwa watoto, ili kuwapatia kinga imara ya mwili ambayo itawafanya kujikinga na magonjwa mbalimbali yatokanayo na upungufu wa kinga mwilini.

Amesema mradi huo ulianza utekelezaji wake Julai mwaka huu na utakoma Juni 2021, ambao unatekelezwa kwenye kata hiyo ya Didia kwa ufadhili wa Shirika la Firelight, ambao walengwa wakuu wa mradi huo ni watoto walio chini ya umri wa miaka sita, ili kuimarisha kinga ya miili yao.

“Tumetoa mafunzo kwa akina mama wa kata hii ya Didia namna ya kuzingatia Lishe bora kwa watoto wao, pamoja na kuwafundisha namna ya kulima viazi Lishe na matumizi yake, ili kuimarisha kinga ya mwili kwa watoto, ambao ndio waathirika wakubwa wa magonjwa mbalimbali ambapo hata virusi vya Corona vilikuwa vikishambulia watoto na wazee,”amesema Myola.

“Elimu ambayo imetolewa leo kwa akina mama hawa 40 kutoka kwa Afisa kilimo, Lishe na wadau wa Lishe, itakwenda kuwa mbegu kwa wenzao ambapo kila mmoja anatakiwa aunde kikundi cha wanawake 10, ili wawe na mashamba darasa ya viazi Lishe, kitendo ambacho kitasaidia kuondoa tatizo la udumavu kwa watoto,”ameongeza.

Naye Afisa Lishe wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mankiligo Said, akitoa elimu hiyo aliwataka akina mama wawe wananyonyesha watoto wao ndani ya miaka miwili ili kuwajengea kinga ya mwili, pamoja na kupika chakula kwa kuzingatia makundi matano ya chakula.

Aidha ametaja hali Lishe katika halmashauri hiyo ya wilaya ya Shinyanga, udumavu ni asilimia 33, ambapo lengo ni kupunguza hali hiyo hadi kufikia asilimia 27 ifikapo mwaka 2025.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Deusi Mhoja, akimwakilisha mkurungezi wa halmashauri hiyo Hoja Mahiba, amelipongeza Shirika hilo la Agape kwa kuendelea kushirikiana na Serikali kutatua changamoto mbalimbali, likiwamo suala la Lishe na ukatili dhidi ya watoto wadogo.

Pia amewataka akina mama hao wakaunde vikundi vya ujasiriamali, ili wapate mkopo wa halmashauri, ambao utawawezesha kulima mashamba makubwa ya viazi Lishe, na kuwaingizia kipato na kukuza uchumi wa familia zao, licha ya kutumia kwa matumizi ya chakula.


TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Mkurugenzi wa Shirika la AGAPE ACP  John Myola, akizungumza na baadhi ya akina mama wa Kata ya Didia namna ya kuzingatia Lishe bora kwa watoto.

Myola akiendelea kutoa elimu kwa akina mama juu ya Lishe bora kwa watoto.

Afisa miradi kutoka Shirika la Agape Peter Amani, akielezea madhumuni ya mradi wa Lishe dhidi ya watoto katika kata ya Didia.

Afisa Tathimini na ufuatiliaji kutoka Shirika la Agape Prosper Ndaiga, akizungumza kwenye mafunzo hayo ya Lishe bora kwa watoto.

Afisa Kilimo wa Kata ya Didia Wiliamu Kuya, akitoa elimu namna ya kulima viazi Lishe.

Afisa Kilimo wa Kata ya Didia Wiliamu Kuya, akitoa elimu namna ya kulima viazi Lishe.

Afisa Lishe halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mankiligo Said, akitoa elimu namna ya kuzingatia Lishe bora kwa watoto na faida zake.

Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Didia Felista Melli, akizungumza kwenye mafunzo hayo ya Lishe.

Afisa maendeleo Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Deus Mhoja, akizungumza kwenye mafunzo hayo ya Lishe bora kwa watoto.

Mdau wa Lishe bora kutoka Shirika lisilo la kiserikali Singida (SMCCT) Evelyne Lyimo, akitoa elimu ya Lishe bora na namna ya kutengeneza viazi Lishe , na kuvitumia katika matumizi mbalimbali ya kula ikiwamo kutengeneza juice, na maandazi.

Elimu ikiendelea kutolewa.

Akina mama wakisikiliza elimu ya Lishe bora kwa watoto na matumizi ya viazi Lishe.

Elimu ya Lishe bora ikiendelea kusikilizwa.

Elimu ya Lishe bora ikiendelea kusikilizwa.

Afisa maendeleo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Deus Mhoja (kulia) akiangalia Unga wa Lishe bora unaotokana na viazi Lishe.

Mdau wa Lishe bora kutoka Shirika lisilo la kiserikali lililopo Singida (SMCCT) Evelyne Lyimo, akiwa ameshika viazi Lishe , kabla ya kuanza kutoa elimu namna ya kuvitengeza kwa matumizi ya juice na maandazi.

Muonekano wa viazi Lishe.

Akina mama wakiendelea na mafunzo ya kutengeneza juice itokanayo na viazi Lishe.

Akina mama wakikanda viazi Lishe kwa ajili ya kutengeneza maandazi.

Zoezi la utengenezaji maandazi kwa viazi Lishe likiendelea.

Akina mama wakipika maandazi yatokanayo na viazi Lishe.

Mkurugenzi wa Shirika la Agape John Myola , akisimamia zoezi hilo la upikaji maandazi yatokanayo na viazi Lishe.

Afisa maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Deus Mhoja, (kushoto) akimkabidhi usafiri wa baiskeli Chausiku Salehe, (katikati) ambaye ni mhudumu wa afya ngazi ya jamii Kata ya Didia ambayo imetolewa na Shirika la Agape kwa ajili ya kuwarahisishia usafiri wa shughuli zao za ulinzi wa mtoto ikiwamo masuala ya afya, (kulia) ni Mkurugenzi wa Agape John Myola.

Wahudumu wa afya ngazi ya jamii 10 kutoka Kata ya Didia wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kukabidhiwa usafiri wa baiskeli na Shirika la Agape.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527