WAZIRI UMMY ASHIRIKI HARAMBEE KANISA LA ANGLIKANA CHUMBAGENI TANGA,ATOA NENO KWA VIONGOZI WA DINI


WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza wakati alipoongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanga Mtaa wa Mtakatifu Augustino wa Hippo Chumbageni Tanga kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kushoto ni Canon Rev Chistopher Kiango ambaye ni Kasisi kiongozi wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanga 
Canon Rev Chistopher Kiango ambaye ni Kasisi kiongozi wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanga  akizungumza wakati wa harambee hiyo
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa halfa hiyo
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto akipokea zawadi ya kuku kutoka kwa Katibu wa Kanisa Anglikana Dayosisi ya Tanga Mtaa wa Mt.Augustino wa Hippo Chumbageni Tanga

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto akipokea mchango wa mtoto Nicolaus Galula wakati wa harambee hiyo


MENEJA wa Hotel ya Tanga Beach ya Jijini Tanga Joseph Ngoyo akizungumza jambo wakati wa harambee hiyo
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto akipokea mchango kutoka kwa Catherine Kitandula wakati wa harambee hiyo
Kwaya ikitumbuiza wakati wa harambee hiyo
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewataka viongozi wa dini kote nchini kuendelea kuliombea Taifa amani, umoja na mshikamano kuelekea uchaguzi mkuu.


Ummy aliyasema hayo leo wakati alipoongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanga Mtaa wa Mtakatifu Augustino wa Hippo Chumbageni Tanga.


Katika harambee hiyo walifanikiwa kukusanya fedha taslimu milioni 13.7 papo hapo na ahadi ikiwa ni milioni 47.2.huku mwisho wa kukusanya michango hiyo ikiwa ni Septemba 20 mwaka huu. 

Katika harambee hiyo ilihudhuriwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa na viongozi wa dini wakiwemo waumini huku kwaya mbalimbali zikitumbuikiza.


“Lakini pia tunawashukuru viongozi wa dini kwa jinsi walivyotuunga mkono kwa sala za kila siku katika mapambano dhidi ya Corona na mungu akatuepusha na janga hili hivyo niwaombe hata wakati huu nchi ikielekea kwenye uchaguzi mkuu tuendelee kuiombea nchi”Alisema Waziri Ummy,


“Nimekuwa nikipata ujumbe kutoka kwa mawaziri wa nchi nyengine Afrika tumefanya kitu gani mpaka hakuna Corona nisema kwamba ugonjwa huo umetoweka kutokana na Mungu ameipenda Tanzania”.


 Awali akisoma risala kwa mgeni rasmi Katibu wa Kanisa hilo Cyprian Mtweve alisema lengo la harambee ya leo katika kuadhimisha sikukuu ya Mt.Agustino wa Hippo ni kupata kiasi cha sh.milioni 125 kwa ajili ya kuezeka kanisa.

 Alisema wanaamini kiasi hicho sio kikubwa kwa Mungu cha kushindwa kupatikana huku wakimshukuru mgeni rasmi kuwaongozea zoezi la harambee hiyo na kushiriki kwa moyo na kwa ukamilifu.

 Aidha alisema upanuzi wa jengo la kanisa hilo umekuwa ukifanywa kwa kulirefusha kwa kiwango ambacho mawasiliano baina ya kasisi anayeongoza ibada madhabahuni na waumini wanaokaa viti vya mwishoni nyuma ya kanisa yanakuwa hafifu kwa sababu ya umbali.

“Jengo hili limejengwa kwa kutumia teknologia ya zamani isiyohimili uwekwaji wa mifumo mbalimbali ya kisasa ikiwemo ile itakayoboresha ibada”,alisema.


Miongoni mwa viongozi ambao wamechangia kwenye harambee hiyo ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Profesa Palamagamba Kabudi wakiwemo wakuu wa wilaya .

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527