WATU 10 WAJERUHIWA AJALI YA LORI NA COSTA MOROGORO


Watu 10 wamejeruhiwa katika ajali ya gari iliyohusisha lori aina ya Scania lenye tela  namba T 394 DHK na Costa ya abiria yenye namba T 147 DHZ,  inayofanya safari za  Mbezi kwenda Morogoro.


Imeelezwa kuwa kati yao, majeruhi wanne wako mahututi, wamepelekwa hospitali.

Akizungumza katika eneo la ajali hiyo, Kamanda wa  Polisi, Willbroad Mutafungwa amesema tela la lori namba T 394 lilikatika katika kiunguo cha kichwa cha lori hilo na kuangukia basi dogo  katika maeneo ya Junior Seminary.

Kamanda Mutafungwa amewataka madereva kuwa makini barabarani.

Dereva wa lori hilo amekimbia na anatafutwa na polisi. Pia, Kamanda wa Jeshi la   Zimamoto na Uokoaji, Goodluck  Zelothe amesema kuwa baada ya kupata taarifa ya ajali hiyo walifika mara moja wakiwa na vifaa vya uokoaji.

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Loata Ole Sanare, amewaonya madereva na wamiliku wa magari kufanya ukaguzi wa magari yao kabla ya kuanza safari barabarani.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527