![]() | ||
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali 30 zilizotolewa na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na usalama kwa ajili ya ujenzi wa Msikiti wa Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma leoAgosti 27, 2020. |
![]() |
Shehe wa Wilaya ya Chamwino Mkoani Bw. Suleiman Matitu akitoa neno la shukrani kwa Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama na Wakuu wa Mikoa waliochangia katika ujenzi wa msikiti wa Wilaya ya Chamwino. |
Sehemu ya malighafi za ujenzi wa msikiti wa Chamwino zikiwa tayari katika eneo la ujenzi wa msikiti wa Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma kama zinavyoonekana.(Picha zote na MAELEZO)
Na
Mwandishi Wetu- Dodoma
Wakuu wa Vyombo vya
Ulinzi na Usalama wamekabidhi Shilingi milioni 30 ujenzi wa msikiti wa kisasa wa Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Akikabidhi mchango
huo leo Agosti 27, 2020 kwa niaba ya wakuu wengine wa vyombo hivyo, Mkuu wa
Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo amesema kuwa wameguswa na
azma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
kuwawezesha wananchi katika masuala mbalimbali ikiwemo ya imani.
“Naamini kuwa
michango zaidi itaendelea kutolewa ili azma ya kujenga msikiti huu ikamilike
kwa wakati”, Alisisitiza Jenerali Mabeyo.
Hafla ya Kukabidhi
fedha hizo imefanyika pembezoni mwa msikiti wa zamani unapojengwa msikiti huo mpya
ambapo Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Jenerali Venance Mabeyo amekabidhi
fedha hizo kwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali, Charles Mbuge, ambaye
ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Suma JKT, inayotekeleza mradi huo.
Naye Mkuu wa Jeshi la
Kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Charles Mbuge amesema kuwa kiasi cha Shilingi milioni 142 zimeshachangwa
na wadau mbalimbali ili kuwezesha ujenzi wa msikiti huo.
Alipongeza jitihada
za kuwafanya watanzania kushikamana bila kujali imani zao kutokana na
ushirikiano ulioneshwa na wadau mbalimbali katika kuchangia ujenzi wa msikiti
huo.
Kwa upande wa Wakuu wa Mikoa yote 26 ya Tanzania Bara,nao
pia wamekabidhi shilingi milioni 26 kwaajili ya Ujenzi huo.
Akizungumza kwa niaba
ya wakuu wa Mikoa hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Evaristi Ndikilo amesema kuwa
wanaunga mkono juhudi za ujenzi wa msikiti huo zilizoanzishwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Aidha, Pamoja na
Fedha hizo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka,amekabidhi shilingi milioni
mbili zilizochangwa na kanisa la AICC la mkoani humo.
Kwa upande wake, Sheikh
mkuu wa Wilaya ya Chamwino Suleiman Matitu
amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli kuchangia ujenzi wa msikiti huo na kuhamasisha wadau mbalimbali
kujitokeza kuchangia.
Aidha, Shehe Matitu
aliwashukuru Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Wakuu wa mikoa kwa kuchangia ujenzi wa msikiti huo.
Azma ya kujenga
msikiti mpya wa Wilaya ya Chamwino ilianzishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli hivi karibuni wakati wa ibada ya Misa
Takatifu katika Kanisa Katoliki la Mt.
Immaculata Chamwino ambapo alizindua kanisa hilo baada ya kuchangia ujenzi wake na ukarabati.
Katika kuendeleza
azma hiyo alianzisha harambee ya ujenzi
wa msikiti huo ambapo hadi sasa kiasi cha Shilingi Milioni 142 zimeshapatikana.
Ujenzi wa Msikiti huo
unatekelezwa na Mkandarasi ambaye ni SUMA JKT na tayari vifaa na malighafi
mbambali zimeanza kufikishwa katika eneo
la ujenzi ili kazi ya ujenzi iweze kuanza mara moja.